Kumbukumbu la Torati 15
15
Amri kuhusu mwaka wa Sabato
1 #
Kut 23:10; Yer 34:14 Kila miaka saba, mwisho wake, fanya maachilio. 2Na jinsi ya maachilio ni hii, kila mkopeshaji na akiache alichomkopesha mwenziwe, wala asimlipize mwenziwe wala nduguye; kwa kuwa imepigwa mbiu ya maachilio ya BWANA. 3#Kum 23:20 Waweza kumtoza mgeni; lakini kila uwiacho kwa nduguyo mkono wako utamwachilia. 4#Kum 28:8 Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa BWANA atakubarikia kweli katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;) 5kwamba utaisikiza tu kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, uyatunze maagizo haya yote nikuagizayo leo, kuyafanya. 6#Mit 22:7 Kwani BWANA, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao.
7 #
Law 25:35; Mt 18:30; 1 Yoh 3:17 Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; 8#Law 25:35; Mt 5:42; Lk 6:34; Gal 2:10 lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo. 9#Kum 28:54; Mit 23:6; 28:22; Mt 20:15; Kum 24:15; Ayu 34:28; Zab 12:5; 140:12; Amo 5:11; Yak 5:4; Mt 25:41 Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako. 10#Mt 25:40; Mdo 20:35; Rum 12:8; 2 Kor 9:5; 1 Tim 6:18; 1 Pet 4:11; Kum 14:29; Zab 41:1; Mit 22:9; 29:7 Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. 11#Mt 26:11; Mk 14:7; Yn 12:8 Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.
12 #
Law 25:39-46; Kut 21:2; Yer 34:14 Ikiwa nduguyo, mume wa Kiebrania, au mwanamke wa Kiebrania, akiuzwa kwako, naye amekutumikia miaka sita; basi mwaka wa saba mwache huru aondoke kwako. 13Nawe utakapomwacha huru aondoke kwako, usimwache aende zake mikono mitupu; 14#Mit 10:22 umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia BWANA, Mungu wako. 15Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, akakukomboa BWANA, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru neno hili hivi leo. 16#Kut 21:5,6 Hata itakuwa, akikuambia, Siondoki kwako; kwa sababu akupenda wewe na nyumba yako, kwa kuwa yu hali njema kwako; 17ndipo utwae uma, uupenyeze katika sikio lake uingie katika ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako milele. Na kijakazi chako naye mfanye vivyo hivyo. 18#Isa 16:14; 21:16 Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na BWANA, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.
Wazaliwa wa kwanza wa wanyama wafugwao
19 #
Kut 13:2
Wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wazaliwao katika kundi lako la ng'ombe na la kondoo, uwatakase kwa BWANA, Mungu wako; usifanye kazi kwa mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wako, wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kundi lako la kondoo. 20#Kum 12:5; 14:23; 16:11 Utamla mbele za BWANA, Mungu wako, mwaka hata mwaka mahali atakapochagua BWANA, wewe na nyumba yako. 21#Law 22:20; Kum 17:1 Lakini akiwa na kilema, akichechea, au akiwa kipofu, au mwenye kilema kibaya chochote, usimsongezee BWANA, Mungu wako, sadaka. 22#Kum 12:15,22 Utamla ndani ya malango yako; wasio tohara na wenye tohara pia watakula, kama unavyokula paa na kulungu. 23#Mwa 9:4; Law 7:26-27; 17:10-14; 19:26; Kum 12:16,23 Pamoja na haya usile damu yake; uimwage nchi kama maji.
Iliyochaguliwa sasa
Kumbukumbu la Torati 15: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: