Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Torati 4

4
Musa awaamuru wawe watiifu
1 # Eze 20:11; Rum 10:5 Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu. 2#Ufu 22:18-19; Kum 12:32; Yos 1:7; Mit 30:6; Mt 15:9 Msiliongeze neno ninalowaamuru wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, ninazowaamuru. 3#Hes 25:1-9 Macho yenu yameona aliyoyatenda BWANA kwa sababu ya Baal-peori; maana wote waliomfuata Baal-peori, BWANA, Mungu wako, amewaangamiza kutoka kati yako. 4Bali ninyi mlioambatana na BWANA, Mungu wenu, mnaishi kila mmoja wenu, hata leo. 5Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki. 6#Ayu 28:28; Zab 19:7; 111:10; Mit 1:7; 2 Tim 3:15; 1 Fal 10:6,9; Dan 1:20; 4:9; Mal 3:12; Mdo 4:13 Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili. 7#2 Sam 7:23; Kut 25:8; 29:45; Law 26:12; 1 Fal 6:13; Zab 46:1; 145:18; Isa 55:6; Zek 2:10; Efe 2:17; Yak 4:8 Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA Mungu wetu alivyo kila tumwitapo? 8Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo? 9#Mit 4:23; 23:19; 3:1,3; 4:21; Mwa 18:19; Kum 6:7; 11:19; Zab 78:5,6; Mit 22:6; Efe 6:4 Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako; 10#Kut 19:9,16; 20:18; Ebr 12:18 siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawafanya wasikilize maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao. 11#Kut 19:16-18; Ebr 12:18-19 Mkakaribia, mkasimama chini ya ule mlima; mlima ukawaka moto mpaka kati ya mbinguni, kwa giza na mawingu, na giza kuu. 12#Kut 20:22; 1 Fal 19:12 BWANA akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lolote; sauti tu. 13#Kut 31:18; 34:28; Kum 9:10 Akawahubiria agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika katika vibao viwili vya mawe. 14#Kut 21:1 BWANA akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki. 15#Yos 23:11; Mit 4:23,27; Yer 17:21; Mal 2:15; Isa 40:18; Mdo 17:24-29 Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yoyote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto; 16#Kut 20:4; Law 26:1; Kum 5:8; 27:15; Rum 1:23 msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yoyote, mfano wa mwanamume au mwanamke, 17#Rum 1:23 mfano wa mnyama yeyote aliye duniani, au mfano wa ndege yeyote arukaye mbinguni, 18au mfano wa kitu chochote kitambaacho juu ya ardhi, au mfano wa samaki yeyote aliye katika maji chini ya nchi; 19#Kum 17:3; Ayu 31:26; Yer 8:2; Mwa 2:1; 2 Fal 17:16; 21:3 tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. 20#Kut 19:5; Kum 7:6; 14:2; 26:18; Tit 2:14; 1 Pet 2:9 Bali BWANA amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuri ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo hivi leo. 21#Hes 20:12 Tena BWANA alinikasirikia kwa ajili yenu, akaapa ya kwamba sitavuka Yordani, na ya kwamba sitaingia nchi ile njema, awapayo BWANA, Mungu wenu, iwe urithi. 22#2 Pet 1:13 Lakini mimi nitakufa katika nchi hii, sina ruhusa kuvuka Yordani; bali ninyi mtavuka, na kuimiliki nchi ile njema. 23Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu chochote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu, 24#Ebr 12:29; Kut 24:17; Kum 9:3; Isa 33:14; Kut 20:5; Kum 6:15; Isa 42:8; 48:11 kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto uangamizao, Mungu mwenye wivu.
25 # 2 Fal 17:17 Utakapozaa wana, na wana wa wana, mkisha kuwa katika nchi siku nyingi, mkajiharibu na kufanya sanamu ya kuchonga kwa umbo la kitu chochote, mkafanya ambayo ni maovu machoni pa BWANA Mungu wako, na kumtia hasira; 26#Kum 30:18,19; Isa 1:2; Mik 6:2 naziita mbingu na nchi hivi leo kushuhudia, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa. 27#Kum 28:36; Law 26:33; Kum 28:62,64; Neh 1:8; Eze 12:15; 32:26 Na BWANA atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu wachache kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na BWANA. 28#Kum 28:36,64; 1 Sam 12:21; Yer 16:13; Eze 20:32,39; Mdo 7:42 Na huko mtatumikia miungu, waliotengenezwa kwa mikono ya watu, miti na mawe, miungu ambao hawaoni, hawasikii, hawali, wala hawanusi. 29#Yer 29:13; 2 Nya 15:4; Neh 1:9; Isa 55:6 Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote. 30#Mwa 49:1; Kum 31:20; Yer 23:20; Hos 3:5; Yer 4:1,2; Yoe 2:12 Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupatwa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia BWANA, Mungu wako, na kuisikiza sauti yake; 31#Kut 34:6; Hes 14:18; 2 Nya 30:9; Neh 9:31; Ayu 8:8; Zab 86:5,15; 103:8; 111:4; Yon 4:2 kwa kuwa BWANA, Mungu wako, ni Mungu wa rehema; hatakuacha wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la baba zako alilowaapia.
32 # Ayu 8:8; Kut 15:11; 1 Sam 2:2; 2 Sam 22:31,32; Isa 44:6,8; 45:5,18; Mt 24:31; Mk 12:29 Tazama siku zilizopita, zilizokuwa kabla yako, tangu siku ile Mungu aliyoumba mwanadamu juu ya nchi, na kutoka pembe hii ya mbingu hadi ile, kama kumetukia neno lolote kama neno hili kubwa, au kwamba kumesikiwa habari ya neno kama hili? 33Je! Kuna wakati wowote watu wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, na wakaendelea kuishi? 34Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa kutoka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, ishara, maajabu, vita, mkono hodari, mkono ulionyoshwa, na vitisho vikuu, kama vile BWANA, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu? 35#Mk 12:29,32; Kum 32:39; 1 Sam 2:2; 2 Sam 22:32; Isa 45:5,18 Wewe umeoneshwa haya, ili upate kujua ya kuwa BWANA ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye. 36#Kut 19:9,19; 20:18,22; 24:16; 1 Nya 29:11; 2 Nya 20:6; Ebr 12:18 Kutoka mbinguni amekufanya usikie sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake kutoka katika moto. 37Na kwa sababu aliwapenda baba zenu, kwa sababu hiyo aliwachagua wazao wao baada yao, akakutoa katika Misri kwa kuwako pamoja nawe, kwa uweza wake mwingi, 38ili kufukuza mbele yako mataifa, walio wakubwa, wenye nguvu kukupita wewe, ili kukuingiza, na kukupa nchi yao iwe urithi, kama ilivyo leo. 39#Yos 2:11; Isa 42:8; Dan 4:35 Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa BWANA ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine. 40#Law 22:31; Kum 5:16; 6:3,18; 12:25,28; 22:7; Efe 6:3 Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako, milele.
Miji ya ukimbizi mashariki mwa Yordani
41 # Yos 20:8-9; Hes 35:6 Ndipo Musa akabagua miji mitatu ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki; 42ili kwamba amwuaye mtu apate kukimbilia huko, amwuaye jirani yake pasipo kujua, wala hakumchukia tangu hapo; ili apate kuishi akimbiliapo mmojawapo miji hiyo; 43nayo ni hii, Beseri ya barani iliyo katika nchi tambarare, kwa Wareubeni; na Ramothi iliyo Gileadi, kwa Wagadi; na Golani iliyo Bashani, kwa Wamanase.
Utangulizi wa sheria ya Mungu
44Na torati Musa aliyowawekea wana wa Israeli ni hii; 45haya ndiyo maagizo, amri na hukumu, Musa alizowaambia wana wa Israeli walipotoka Misri; 46#Kum 3:29 ng'ambo ya Yordani, katika bonde lililoelekea Beth-peori, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni ndiye aliyepigwa na Musa na wana wa Israeli, walipotoka Misri; 47#Hes 21:35; Kum 3:3,4 wakaishika nchi yake, ikawa milki yao, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, ndio wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki; 48#Kum 2:36; 3:12; Zab 133:3 toka Aroeri, iliyo juu ya ukingoni pa bonde la Arnoni, hadi mlima wa Sioni (nao ndio Hermoni), 49na Araba yote iliyo ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, hata mpaka bahari ya Araba, chini ya materemko ya Pisga.

Iliyochaguliwa sasa

Kumbukumbu la Torati 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia