Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 23

23
Ohola na Oholiba
1Neno la BWANA likanijia tena, kusema, 2#Yer 3:7; Eze 16:46 Mwanadamu, palikuwa na wanawake wawili, binti za mama mmoja; 3#Law 17:7; Yos 24:14; Eze 20:8 nao walizini huko Misri; walizini wakati wa ujana wao; huko vifua vyao vilishikwashikwa, na matiti yao yakatomaswa wakapoteza ubikira wao. 4Na majina yao, mkubwa aliitwa Ohola, na dada yake Oholiba; wakawa wangu, wakazaa watoto wa kiume na wa kike. Na katika hayo majina yao, Samaria ni Ohola, na Yerusalemu ni Oholiba. 5#2 Fal 15:19; 16:7; Hos 5:13; 8:9; 10:6 Na Ohola alifanya mambo ya kikahaba alipokuwa wangu; naye alipenda mno wapenzi wake, Waashuri, jirani zake, 6waliovikwa mavazi ya samawati, watawala na mawaziri, wote vijana wa kutamanika, wapanda farasi wakipanda farasi wao. 7Akawagawia mambo yake ya kikahaba, watu wateule wa Ashuru, wote pia; akajitia unajisi kwa vinyago vyote vya kila mmoja wa hao aliowapenda. 8Wala hakuyaacha mambo yake ya kikahaba tangu siku za Misri, kwa maana wakati wa ujana wake walilala naye, wakayabana matiti ya ubikira wake wakamwaga uzinzi wao juu yake. 9#2 Fal 17:3-6,23 Kwa sababu hiyo nilimtia katika mikono ya wapenzi wake, katika mikono ya Waashuri, aliowapendelea. 10#Eze 16:37,41 Na hawa wakaufunua uchi wake, wakatwaa wanawe na binti zake, wakamwua yeye kwa upanga; akawa jina la aibu kati ya wanawake; kwa maana walitoa hukumu juu yake. 11Na dada yake, Oholiba, akayaona hayo lakini alizidi kuharibika kuliko yeye, kwa kupendelea kwake, na kwa uzinzi wake, uliokuwa mwingi kuliko uzinzi wa dada yake. 12#2 Fal 16:7 Aliwapendelea Waashuri, watawala na mawaziri, jirani zake, waliovikwa nguo za shani, wapanda farasi wakipanda farasi wao, wote pia vijana wa kutamanika. 13Nikaona ya kuwa ametiwa unajisi; wote wawili walifuata njia moja. 14#Yer 50:2 Naye akaongeza uzinzi wake; kwa maana aliona wanaume, ambao sura zao zimeandikwa ukutani, sura za Wakaldayo zilizoandikwa kwa rangi nyekundu; 15waliofungiwa mikumbuu viunoni mwao, na vilemba vilivyotiwa rangi vichwani mwao; wote wakuu wa kuangaliwa, kwa mfano wa wana wa Babeli katika Ukaldayo, katika nchi ya kuzaliwa kwao. 16Na mara alipowaona aliwapendelea, akatuma wajumbe kwao hata Ukaldayo. 17Na watu wa Babeli wakamwendea katika kitanda cha mapenzi, wakamtia unajisi kwa uzinzi wao, akatiwa unajisi nao, kisha roho yake ikafarakana nao. 18#Kum 32:19; Zab 78:59; Yer 12:8; 15:1; Omb 2:7; Amo 6:8; Zek 11:8 Basi alipoendelea na ukahaba wake waziwazi, na kufunua uchi wake; ndipo roho yangu ikafarakana naye, kama ilivyofarakana na dada yake. 19Lakini aliongeza uzinzi wake, akikumbuka siku za ujana wake, alipofanya mambo ya kikahaba katika nchi ya Misri. 20#Eze 16:26 Akawapendelea wapenzi wao, ambao nyama ya mwili wao ni kama nyama ya mwili wa punda, nacho kiwatokacho ni kama kiwatokacho farasi. 21Ndivyo ulivyokumbuka uasherati wa ujana wako, yalipobanwa matiti yako na Wamisri, kwa maziwa ya ujana wako.
22 # Isa 10:5,6; Eze 16:37 Kwa sababu hiyo, Ewe Oholiba, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawachochea wapenzi wako juu yako, hao ambao roho yako imefarakana nao, nami nitawaleta juu yako pande zote; 23watu wa Babeli, na Wakaldayo wote, Pekodi na Shoa na Koa, na Waashuri wote pamoja nao; vijana wa kutamanika, wote pia, watawala na mawaziri, wakuu, na watu wenye sifa, wote wenye kupanda farasi. 24#Nah 3:2; 2 Sam 24:14; Yer 47:3; 39:5; Eze 16:38 Nao watakuja kwako na silaha zao, na magari ya vita, na magurudumu, na wingi wa mataifa; watajipanga juu yako kwa ngao, na vigao, na chapeo za shaba, pande zote; nami nitawapa uwezo wa kuhukumu, nao watakuhukumu kulingana na hukumu zao. 25Nami nitaweka wivu wangu juu yako, nao watakutenda mambo kwa ghadhabu; watakuondolea pua yako na masikio yako; na mabaki yako wataanguka kwa upanga; watawatwaa wanao na binti zako; na mabaki yako watateketea motoni. 26#Yer 13:22; Eze 16:39; Ufu 17:16 Pia watakuvua nguo zako, na kukunyang'anya johari zako uzuri. 27#Eze 16:41; Mik 5:10 Hivyo ndivyo nitakavyoukomesha uasherati wako, na uzinzi wako, ulioletwa toka nchi ya Misri; usije ukawainulia macho yako, na kukumbuka Misri tena. 28#Yer 21:7; Eze 16:37 Maana Bwana MUNGU asema hivi, Tazama nitakutia katika mikono yao unaowachukia, katika mikono yao, ambao roho imefarakana nao; 29#Eze 16:39 nao watakutenda mambo kwa chuki, watakunyang'anya matunda yote ya kazi yako, watakuacha uchi, huna nguo na aibu ya mambo yako ya kikahaba itafunuliwa, uasherati wako na uzinzi wako. 30#Eze 6:9 Utatendwa mambo hayo kwa sababu umezini na hao wasioamini, na kwa sababu umetiwa unajisi kwa vinyago vyao. 31#Zab 11:6; Yer 25:15; Dan 9:12 Umekwenda katika njia ya dada yako; basi nitatia kikombe chake katika mkono wako. 32#Kum 28:37; Eze 22:4,5 Bwana MUNGU asema hivi; Utakinywea kikombe cha dada yako; chenye kina kirefu na kipana; utadhihakiwa na kudharauliwa; nacho kimejaa sana. 33Utajazwa ulevi na sikitiko, kwa kikombe cha ushangao na ukiwa, kikombe cha dada yako Samaria. 34#Zab 75:8; Isa 51:17 Naam, utakinywea hata hakitabaki kitu ndani yake, utavitafuna vigae vyake, utayararua maziwa yako; maana mimi, Bwana MUNGU, nimenena neno hili. 35#Yer 2:32; 3:21; 1 Fal 14:9; Neh 9:26 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa umenisahau, na kunitupa nyuma yako, basi kwa hiyo, uchukue uasherati wako na uzinzi wako.
36 # Isa 58:1 Tena BWANA akaniambia, Mwanadamu, utawahukumu Ohola na Oholiba? Basi watangazie matendo yao maovu. 37#Eze 16:20,38 Maana wamezini, na damu imo mikononi mwao, nao wamezini na vinyago vyao; tena wana wao walionizalia wamewapitisha katika moto ili waliwe nao. 38#Eze 22:8 Tena wamenitenda haya; wamepatia unajisi mahali pangu patakatifu, siku ile ile, nao wamezitangua sabato zangu. 39#2 Fal 21:4; Yer 23:11; Eze 44:7 Kwa maana walipokuwa wamekwisha kuvichinjia vinyago vyao watoto wao, ndipo walipoingia patakatifu pangu, siku ile ile, wapatie unajisi, na tazama, wamefanya hivyo katika nyumba yangu. 40#Isa 57:9; Rut 3:3; 2 Fal 9:30; Yer 4:30 Tena mmewatuma watu kuwaita watokao mbali; ambao mjumbe alitumwa kwao, na tazama, wakaja; nawe ulijiosha kwa ajili yao, ulitia rangi macho yako, na kuremba kwa mapambo mazuri; 41#Mit 7:17; Yer 44:17; Eze 16:18,19; Hos 2:8 ukaketi juu ya kitanda cha enzi, na meza imeandikwa tayari mbele yake, ambayo juu yake uliweka uvumba wangu na mafuta yangu. 42Na sauti za wingi wa watu wenye hali ya raha zilikuwa pamoja naye; na pamoja na watu wasio na adabu, waliletwa walevi toka jangwani; wakawatia vikuku mikononi, na taji zuri juu ya vichwa vyao. 43Ndipo nikasema, Huyo aliye mkongwe atafanya uzinzi! Sasa hao watazini naye, naam, na yeye! 44Wakamwingilia kama watu wamwingiliavyo kahaba; ndivyo walivyowaingilia Ohola na Oholiba, wanawake wale waasherati. 45#Eze 16:38; Yn 8:4-7 Basi watu wenye haki watawahukumu, kwa hukumu iwapasayo wazinzi, na kwa hukumu iwapasayo wanawake wamwagao damu; kwa sababu wao ndio wazinzi, na mikononi mwao mna damu. 46Maana Bwana MUNGU asema hivi; Nitaleta kusanyiko la watu juu yao, nami nitawatoa warushwe huku na huko, na kutekwa nyara. 47#Eze 16:41; 24:21; 2 Nya 36:17 Na kusanyiko hilo watawapiga kwa mawe, na kuwaua kwa panga zao; watawaua wana wao na binti zao, na kuziteketeza nyumba zao kwa moto. 48#Kum 13:11; 2 Pet 2:6 Hivyo nitaukomesha uasherati katika nchi hii, ili wanawake wote wafundishwe, wasifanye uasherati kama mlivyofanya. 49Nao watawalipa ninyi malipo ya uasherati wenu, nanyi mtachukua dhambi za vinyago vyenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.

Iliyochaguliwa sasa

Ezekieli 23: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia