Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 3:16-27

Ezekieli 3:16-27 SRUV

Hata ikawa, mwisho wa siku saba, neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu. Nikimwambia mtu mwovu, Hakika utakufa; na wewe usimpe maonyo, wala kusema na huyo mtu mwovu ili kumwonya, ili kusudi aache njia yake mbaya na kuiokoa roho yake; mtu yule mwovu atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mwovu, wala yeye hauachi uovu wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako. Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikaweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikawa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu alikubali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako. Na mkono wa BWANA ulikuwako juu yangu huko; akaniambia, Ondoka, nenda bondeni; nami nitasema nawe huko. Basi, nikaondoka, nikaenda bondeni, na tazama, utukufu wa BWANA ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi. Ndipo roho ile ikaniingia, ikanisimamisha kwa miguu yangu; akasema nami, akaniambia, Nenda ukajifungie nyumbani mwako. Lakini wewe, mwanadamu, tazama, watakutia pingu, nao watakufunga kwazo, wala hutakwenda nje kati yao; nami nitaufanya ulimi wako ugandamane na kaakaa lako, hata utakuwa bubu, wala hutakuwa mwonyaji kwao; kwa kuwa wao ni nyumba yenye kuasi. Lakini hapo nitakaposema nawe, nitafumbua kinywa chako, nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi. Yeye asikiaye na asikie; naye akataaye na akatae; maana wao ni nyumba yenye kuasi.

Soma Ezekieli 3

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ezekieli 3:16-27