Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 13

13
Kutengana kwa Abramu na Lutu
1Abramu akapanda kutoka Misri, yeye, na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini. 2#Mwa 24:35; Zab 112:3; Mit 10:22 Naye Abramu alikuwa tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu. 3Akaendelea kusafiri kutoka kusini mpaka Betheli, mahali pale palipokuwapo hema yake kwanza, kati ya Betheli na Ai; 4#Mwa 12:7,8 napo ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo kwanza; naye Abramu akaliitia jina la BWANA hapo. 5Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema. 6#Mwa 36:7; Lk 12:17,18 Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja. 7#Mwa 26:20 Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi. 8#Flp 2:14,15; Zab 133:1 Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu jamaa moja. 9#Mwa 20:15; Rum 12:18; Ebr 12:14; Yak 3:13-18 Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi jitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kulia; ukienda upande wa kulia, nitakwenda upande wa kushoto. 10#Mwa 2:10; Hes 32:1; Kum 34:3; Zab 107:34; Mwa 14:2; 19:22,24 Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari. 11Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao. 12#Mwa 19:29 Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma. 13#Mwa 6:11; 18:20; Eze 16:49; 2 Pet 2:7 Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA.
14 # Isa 49:18; Mwa 28:14 BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; 15#Mdo 7:5; 2 Nya 20:7 maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. 16#Mwa 26:4; Kut 32:13; Hes 23:10; Kum 1:10; 1 Nya 27:23; Yer 33:22; Rum 4:16; Ebr 11:12 Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; ikiwa mtu ataweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika. 17Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo. 18Basi Abramu akahamisha hema yake, akaja na kukaa karibu na mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 13: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia