Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 7:18-25

Waraka kwa Waebrania 7:18-25 SRUV

Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake; (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo tunamkaribia Mungu. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo, (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;) basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu walizuiliwa na mauti wasikae; bali yeye, kwa kuwa anakaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Waraka kwa Waebrania 7:18-25