Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 14

14
Mwito wa kutubu
1 # 1 Sam 7:3,4; Hos 12:6; Isa 55:6,7 Ee Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako. 2#Yoe 2:17; Rum 8:26; Ebr 13:15 Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie BWANA; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng'ombe. 3Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.
Tumaini la kusamehewa
4Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha. 5Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni. 6Matawi yake yatatanda, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni. 7Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni. 8#Yer 31:18; Yak 1:17 Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.
9 # Yn 18:37; Mt 11:19 Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.

Iliyochaguliwa sasa

Hosea 14: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia