Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 4

4
Mungu ailaumu Israeli
1 # Mik 6:2; Yer 4:22 Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. 2Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na kumwaga damu mfululizo. 3#Amo 8:8; Sef 1:3 Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa porini na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataangamizwa.
4 # Kum 17:12 Lakini asishindane mtu, wala mtu asikemee; maana watu wako ni kama wao washindanao na kuhani. 5#Yer 6:4 Na wewe utajikwaa wakati wa mchana, na nabii naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku; nami nitamwangamiza mama yako. 6Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. 7Kadiri walivyozidishwa, kwa kadiri iyo hiyo walinitenda dhambi; nami nitageuza utukufu wao kuwa aibu. 8Hujilisha dhambi ya watu wangu, hujifurahisha moyo kwa uovu wao. 9Hata itakuwa, kama walivyo watu, ndivyo atakavyokuwa kuhani; nami nitawaadhibu kwa ajili ya njia zao, na kuwalipa kwa matendo yao.
10 # Mik 6:14; Hag 1:6 Nao watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka; kwa sababu wameacha kumwangalia BWANA.
Uzinzi wa Israeli
11 # Isa 28:7 Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu. 12#Yer 2:27; Isa 44:20; Ufu 17:2 Watu wangu hutaka shauri kwa kipande cha mti, na fimbo yao huwatolea uaguzi; maana roho ya uzinzi imewapotosha, wakawacha Mungu wao. 13#Ayu 31:9,10; Amo 7:17; Rum 1:28 Hutoa dhabihu juu ya vilele vya milima, na kufukiza uvumba juu ya vilima, chini ya mialoni na milibua na miela, kwa kuwa uvuli wake ni mwema; kwa sababu hiyo binti zenu huzini, na bibi arusi zenu hufanya uasherati. 14Sitawaadhibu binti zenu wazinipo, wala bibi arusi zenu wafanyapo uasherati; maana wenyewe huenda kando pamoja na wanawake wazinzi, hutoa dhabihu pamoja na makahaba; na watu hawa wasiofahamu wataangamia.
15 # Hos 9:15; Amo 4:4; 8:14 Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo BWANA. 16Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! BWANA atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye malisho mazuri.#4:16 Katika Kiebrania ni penye nafasi. 17#Mit 15:14 Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache. 18Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu. 19Upepo umemfunika kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao.

Iliyochaguliwa sasa

Hosea 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia