Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 7

7
1Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwizi huvunja nyumba za watu, na kundi la magaidi hushambulia nje. 2#Mit 5:22; Zab 90:8 Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu. 3#Rum 1:32 Humfurahisha mfalme kwa uovu wao, na wakuu wao kwa uongo wao. 4Hao wote ni wazinzi; wamekuwa kama tanuri iliyotiwa moto na mwokaji; asiyehitajika kuuchochea moto, tangu kuukanda unga hadi utakapokwisha kutiwa chachu. 5Sikukuu ya mfalme wetu, wakuu waliugua kwa ukali wa divai; alinyosha mkono wake pamoja na wenye mzaha. 6Maana wamefanya moyo wao kuwa tayari kama tanuri, wakati waoteapo; hasira yao hulala usiku kucha; asubuhi yawaka kama moto utoao miali. 7#2 Fal 15:10; Isa 9:13 Wote wamepata moto kama tanuri, nao hula watawala wao; wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao aniitaye mimi. 8#Zab 106:35 Efraimu ajichanganya na mataifa; Efraimu ni mkate usiogeuzwa. 9Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huku na huko juu yake, naye hana habari.
10Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia BWANA, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.
Tegemeo batili kutoka kwa mataifa
11Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru. 12#Law 26:14 Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia. 13Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu. 14#Ayu 35:9; Zab 78:34-37; Isa 29:13; Yer 3:10 Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi. 15Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu. 16#Zab 73:9 Wao hurudi, lakini si kwake Aliye Juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya ujeuri wa ndimi zao; na kwa sababu hiyo watachekwa katika nchi ya Misri.

Iliyochaguliwa sasa

Hosea 7: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia