Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 27

27
Ukombozi wa Israeli
1 # Eze 29:3; Ayu 41:1; Zab 74:14; 104:26 Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu Lewiathani, nyoka yule mwepesi, na Lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule joka aliye baharini. 2Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.
3Mimi, BWANA, nililinda,
Nitalitia maji kila dakika,
Asije mtu akaliharibu;
Usiku na mchana nitalilinda.
4 # 2 Sam 23:6 Mimi sina hasira ndani yangu;
Kama mbigili na miiba ingekuwa mbele zangu,
Ningepanga vita juu yake,
Ningeiteketeza yote pamoja.
5 # Ayu 22:21; Isa 53:4,5; Efe 2:12-14 Au azishike nguvu zangu,
Afanye amani nami;
Naam, afanye amani nami.
6 # Isa 37:31; Hos 14:5,6 Siku zijazo Yakobo atatia mizizi;
Israeli atatoa maua na kuchipuka;
Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
7Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye? 8#Ayu 23:6; Zab 6:1; Yer 10:24; 1 Kor 10:13 Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki. 9Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena. 10#Isa 17:2 Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake. 11#Kum 32:18,28; Zab 28:5; Isa 1:3; 44:2,21,24; Yer 4:22; 2 The 1:8 Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
12Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA atayapigapiga matunda yake toka gharika ya Mto hadi kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
13 # Isa 2:11; Hes 10:2; Zab 81:3; Hos 8:1; Mt 24:31; Ufu 11:15 Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 27: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia