Waamuzi 1
1
Waisraeli washindwa kuiteka Kanaani yote
1 #
Kut 28:30; Hes 27:21; Amu 20:18; 1 Sam 23:9 Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza BWANA, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao? 2#Mwa 49:8 BWANA akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake. 3#Mhu 4:9; Mk 6:7; 1 Kor 12:26; Gal 6:2 Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika eneo langu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika eneo lako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye. 4#Kum 9:1; Zab 44:2; 78:55 Yuda akakwea; naye BWANA akawatia Wakanaani na Waperizi mkononi mwao; nao wakawapiga huko Bezeki watu elfu kumi. 5Wakampata huyo Adoni-bezeki huko Bezeki; wakapigana naye, nao wakawapiga Wakanaani na Waperizi. 6Lakini Adoni-bezeki akakimbia; nao wakamwandama na kumshika, wakamkata vidole vyake vya gumba vya mikono na vya miguu. 7#Law 24:19; Zab 109:16; Mit 1:31; Mk 4:24; Yak 2:13 Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vidole vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo hivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko.
8 #
Yos 15:63
Kisha wana wa Yuda wakapigana na Yerusalemu, wakautwaa, wakaupiga kwa makali ya upanga, na kuupiga moto huo mji. 9#Yos 10:12,36; 11:21 Baadaye wana wa Yuda wakateremka ili wapigane na hao Wakanaani waliokaa katika nchi yenye milima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela. 10#Yos 14:15 Kisha Yuda akawafuatia hao Wakanaani waliokaa katika Hebroni; (jina la Hebroni hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-arba;) nao wakamwua Sheshai, na Ahimani, na Talmai. 11#Yos 15:15 Kisha kutoka hapo akawafuatia wale wenye kukaa Debiri. (Jina la Debiri hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-seferi.) 12Huyo Kalebu alisema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, nitamwoza mwanangu Aksa awe mkewe. 13#Amu 3:9 Naye Othnieli, mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa huyo Kalebu, aliutwaa; basi akamwoza mwanawe Aksa. 14#Yos 15:18 Ikawa hapo alipokwenda kukaa naye, huyo mwanamke akamtaka ili aombe shamba kwa baba yake; na huyo mwanamke akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Una haja gani utakayo? 15#Mwa 33:11; 1 Sam 25:27; Ebr 6:7 Mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa wewe umeniweka katika nchi ya Negebu, basi unipe na vijito vya maji pia. Kalebu akampa vile vijito vya maji vya juu na vijito vya chini.
16 #
Hes 10:29-32; 24:21,22; Amu 4:11; 1 Sam 15:6; 1 Nya 2:55; Yer 35:2; Kum 34:3; 2 Nya 28:15; Hes 21:1; 10:32 Hao wana wa Mkeni, huyo shemeji yake Musa, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao. 17#Hes 21:3; Yos 19:4 Kisha Yuda akaenda pamoja na nduguye Simeoni, na wakawapiga Wakanaani waliokaa katika Sefathi, na kuuharibu mji kabisa. Na jina la mji huo ulikuwa ukiitwa Horma. 18#Yos 11:22; 13:3; 15:47; Amu 16:1; 1 Sam 6:17 Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake. 19#Mwa 39:21; Yos 1:5,9; 14:12; 2 Sam 5:10; 2 Fal 18:7; Rum 8:31; Yos 17:16 BWANA alikuwa pamoja na Yuda; naye akawafukuza watu waliokaa katika nchi yenye milima; asiweze kuwafukuza hao waliokaa katika hilo bonde, kwa kuwa wao walikuwa na magari ya chuma. 20#Yos 15:13-14; Hes 14:24; Kum 1:36; Yos 14:9,13 Kisha wakampa huyo Kalebu Hebroni, kama alivyonena Musa naye akawafukuza wale wana watatu wa Anaki. 21#Yos 15:63; 18:28; 2 Sam 5:6; 1 Nya 11:4 Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa mji wa Yerusalemu; bali Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Benyamini ndani ya Yerusalemu hata hivi leo.
22Nyumba ya Yusufu nayo, wao nao walikwea kwenda juu ya Betheli; naye BWANA alikuwa pamoja nao. 23#Yos 2:1; 7:2; Amu 18:2; Mwa 28:19 Kisha watu wa ukoo wa Yusufu wakatuma watu waende kuupeleleza Betheli. (Jina la mji huo hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Luzu.) 24#Yos 2:12; 1 Sam 30:15 Hao wapelelezi walimwona mtu atoka katika huo mji, wakamwambia, Tafadhali, utuoneshe njia ya kuingia mji huu, nasi tutakutendea mema. 25Basi akawaonesha njia ya kuingia mji, nao wakaupiga huo mji kwa makali ya upanga; lakini huyo mtu walimwacha aende zake, na watu wote wa jamaa yake. 26Huyo mtu akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji, akaliita jina la huo mji Luzu; nalo ndilo jina lake hata hivi leo.
27 #
Yos 17:11-13; 21:25 Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Beth-sheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo. 28Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepata nguvu, ndipo walipowatia hao Wakanaani katika kazi ya shokoa, wala hawakuwafukuza kabisa.
29 #
Yos 16:10; 1 Fal 9:16 Efraimu naye hakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa katika Gezeri; lakini Wakanaani walikaa ndani ya Gezeri kati yao.
30 #
Yos 19:15
Zabuloni naye hakuwatoa wenyeji wa Kitroni, wala hao waliokaa katika Nahalali; lakini Wakanaani walikaa kati yao, wakalazimishwa shokoa.
31 #
Yos 19:24-30
Asheri naye hakuwatoa wenyeji wa Aka, wala hao waliokaa Sidoni, wala hao wa Alabu, wala hao wa Akzibu, wala hao wa Helba, wala hao wa Afeka, wala hao wa Rehobu; 32#Zab 106:34,35 lakini Waasheri wakakaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; kwa kuwa hawakuwafukuza.
33 #
Yos 19:38
Naftali naye hakuwatoa wenyeji wa Beth-shemeshi, wala hao waliokaa Bethanathi; lakini alikaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; pamoja na haya, hao wenyeji wa Beth-shemeshi, na wenyeji wa Bethi-anathi, wakawatumikia kazi ya shokoa.
34Kisha Waamori waliwasukumiza wana wa Dani waende milimani; kwani hawakuwakubali kuteremkia bondeni; 35#Yos 10:12; 19:42; Amu 12:12 lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa. 36#Hes 34:4; Yos 15:3 Mpaka wa Waamori ulikuwa tangu huko kupandia Akrabimu, tangu hilo jabali, na juu yake.
Iliyochaguliwa sasa
Waamuzi 1: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: