Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waamuzi 3

3
Mataifa yasalimishwa
1 # Mwa 22:1; Kum 8:2,16; 13:3; Yn 2:24; 1 Kor 11:19 Basi haya ndiyo mataifa ambao BWANA aliwaacha, ili awajaribu Israeli kwa hao, yaani, awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kanaani; 2ili kwamba vizazi vya wana wa Israeli wapate kujua ili kuwafundisha vita, hasa wao ambao hawakujua vita kabla ya wakati ule; 3#Yos 13:3 aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi. 4Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua kwamba watasikiliza amri za BWANA, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa. 5#Zab 106:35 Basi wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao Wahiti, na hao Waamori, na hao Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi; 6#Kut 34:16; Kum 7:3; Ezr 9:11 wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe wakawaoza wana wao waume, na kuitumikia miungu yao.
Othnieli
7 # Amu 2:11; Kut 34:13; Kum 16:21; Amu 6:25 Wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, nao wakamsahau BWANA, Mungu wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtorethi. 8#Hab 3:7 Kwa hiyo hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane. 9#Amu 6:7; 10:10; 1 Sam 12:10; Neh 9:27; Zab 22:5; 106:44; Amu 2:13,16 Kisha wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu. 10#Hes 11:17; 27:18; 1 Sam 10:6; 11:6; 16:13; 2 Nya 15:1; Ebr 6:4 Roho ya BWANA ikamjia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kuenda vitani, naye BWANA akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu. 11Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka arubaini. Kisha Othnieli, mwana wa Kenazi, akafa.
Ehudi
12 # Amu 2:19; Yer 16:12; Hos 6:4; Mt 23:32; 1 Sam 12:9 Basi wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu tena mbele za BWANA; naye BWANA akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli, kwa sababu walikuwa wameyafanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA. 13#Amu 5:14; Kum 34:3; Amu 1:16 Huyo Egloni akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao wakauchukua huo mji wa mitende. 14#Law 26:23-25; Kum 28:40 Wana wa Israeli walimtumikia Egloni mfalme wa Moabu muda wa miaka kumi na minane. 15#Zab 50:15; 78:34; Yer 29:12,13; Dan 9:3; Amu 20:16 Lakini wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi. 16Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kulia. 17Kisha akamsogezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyenenepa sana. 18Naye hapo alipomaliza kuitoa hiyo tunu, akawapa ruhusa watu hao walioichukua tunu, wakaenda zao. 19#Yos 4:20 Lakini yeye mwenyewe akageuka kutoka huko kwenye sanamu zilizokuwa karibu na Gilgali, akasema, Mimi nina ujumbe wa siri kwako wewe, Ee mfalme. Naye akasema, Nyamazeni kimya. Watu wote waliokuwa wanasimama karibu naye wakatoka na kumwacha. 20Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, “Nina ujumbe wako kutoka kwa Mungu”. Basi akainuka katika kiti chake. 21Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kulia, akamtia tumboni mwake; 22hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma.#3:22 Maana ya neno la Kiebrania si dhahiri. 23Ndipo Ehudi akatoka nje barazani,#3:23 Maana yake katika Kiebrania si dhahiri. akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo. 24Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi ameenda haja#3:24 Katika Kiebrania ni kufunika miguu. ndani ya chumba cha baridi. 25Wakangoja hadi wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka chini, naye amekufa. 26Naye Ehudi alikimbia hapo walipokuwa wakingoja, Ehudi alitoroka kwa kupitia huko kwenye sanamu, na kukimbilia Seira. 27#Amu 5:14; 6:34; 1 Sam 13:3; Yos 17:15; Amu 7:24; 17:1 Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia. 28#Amu 7:9,15; 1 Sam 17:47; Yos 2:7; Amu 12:5 Akawaambia, Nifuateni; kwa kuwa BWANA amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakateremka na kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha mtu kuvuka. 29Wakati huo wakawaua Wamoabi wapatao wanaume elfu kumi, ambao wote walikuwa wenye nguvu na mashujaa, hakunusurika hata mtu mmoja. 30Basi Moabu alishindwa siku hiyo chini ya mikono ya Israeli. Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka themanini.
Shamgari
31 # 1 Sam 17:47,50; Amu 2:16 Tena baada ya Ehudi#3:31 Katika Kiebrania ni ‘yake huyo’. alikuwapo Shamgari mwana wa Anathi, aliyewaua Wafilisti watu mia sita kwa fimbo ya kuswagia ng'ombe; naye aliwaokoa Israeli.

Iliyochaguliwa sasa

Waamuzi 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia