Ayubu 20
20
Sofari anena: Uovu hupatilizwa ipasavyo
1Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema,
2Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu,
Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu.
3Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha,
Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu.
4Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale,
Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,
5 #
Zab 37:35
Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo,
Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?
6Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni,
Na kichwa chake kufikia mawinguni;
7Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe;
Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?
8Ataruka mfano wa ndoto, asionekane;
Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,
9Jicho lililomwona halitamwona tena;
Wala mahali pake hapatamtazama tena.
10Watoto wake watataka fadhili kwa maskini,
Na mikono yake itarudisha mali yake.
11Mifupa yake imejaa ujana wake,
Lakini utalala nchi naye mavumbini.
12Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake,
Ingawa auficha chini ya ulimi wake;
13Ingawa hawataki kuuachilia uende zake.
Naye huushikilia kinywani mwake;
14 #
Yer 4:18
Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika,
Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.
15 #
Mt 27:3,4 Amemeza mali, naye atayatapika tena;
Mungu atayatoa tumboni mwake.
16Atanyonya sumu ya majoka;
Na ulimi wa fira utamwua.
17 #
Yer 17:6
Hataiangalia hiyo mito ya maji,
Vile vijito vilivyojaa asali na siagi.
18Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze;
Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi.
19Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini;
Amenyang'anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga.
20 #
Mhu 5:13
Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake,
Hataokoa chochote kutoka hicho alichokifurahia.
21Hakikusalia kitu asichokula;
Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu.
22Katika kujaa kwa wingi wake atakuwa katika dhiki;
Mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia.
23 #
Hes 11:33; Zab 78:30,31 Hapo atakapo kulijaza tumbo lake,
Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake,
Na kuunyesha juu yake akiwa anakula.
24 #
Isa 24:18; Yer 48:43; Amo 5:19 Ataikimbia silaha ya chuma,
Na uta wa shaba utamchoma.
25 #
Ayu 18:11; Zab 73:19 Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake;
Naam, ncha ing'aayo yatoka katika nyongo yake;
Vitisho viko juu yake.
26 #
Zab 21:9
Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake;
Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla;
Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake.
27 #
Isa 26:21
Mbingu zitafunua wazi uovu wake,
Nayo nchi itainuka kinyume chake.
28Mali ya nyumba yake yatanyakuliwa,
Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake.
29 #
Kum 29:20,28; Ayu 18:21; 27:13; Zab 11:5,6; Mt 24:51 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu,
Na urithi aliowekewa na Mungu.
Iliyochaguliwa sasa
Ayubu 20: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: