Ayubu 29
29
Ayubu amalizia hoja zake
1Kisha Ayubu akaendelea na hoja yake, na kusema,
2Laiti ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi ya zamani,
Kama katika siku hizo Mungu aliponilinda;
3 #
Ayu 18:6; Zab 18:28 Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani,
Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;
4 #
Zab 25:14; Mit 3:32 Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa,
Hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu;
5Wakati Mwenyezi alipokuwa angali pamoja nami,
Nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka;
6 #
Mwa 49:11; Kum 32:13; Zab 81:16 Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi,
Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta!
7Wakati nilipotoka kwenda mjini, kupitia langoni,
Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,
8Hao vijana waliniona wakanipisha,
Nao wazee wakasimama kwa heshima;
9Wakuu wakanyamaa wasinene,
Na kuweka mikono yao vinywani mwao;
10 #
Zab 137:6
Sauti yao wakuu ilinyamaa,
Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao.
11Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia;
Na jicho liliponiona, likanishuhudia.
12 #
Zab 72:12; Mit 21:13 Kwa sababu nilimwokoa maskini aliyenililia;
Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
13Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia;
Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
14 #
Zab 132:9; Rum 13:14; Efe 6:14 Nilijivika haki, ikanifunika,
Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.
15 #
Hes 10:31
Nilikuwa macho kwa kipofu,
Nilikuwa miguu kwa aliyechechemea.
16 #
Mit 29:7
Nilikuwa baba kwa mhitaji,
Na kesi ya mtu nisiyemjua niliichunguza.
17Nami nilizivunja taya za wasio haki,
Na kumpokonya mawindo katika meno yake.
18 #
Zab 30:6
Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kiota changu,
Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga;
19 #
Zab 1:3; Yer 17:8 Shina langu limeenea hata kufika majini,
Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;
20 #
Mwa 49:24
Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu,
Na uta wangu hurejeshwa upya mkononi mwangu.
21Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja,
Wakanyamaza kimya wapate kusikia mashauri yangu.
22Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu;
Matamko yangu yakadondoka juu yao.
23Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua;
Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika.
24Walipokata tamaa nikacheka nao;
Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha.
25Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao.
Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari,
Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.
Iliyochaguliwa sasa
Ayubu 29: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: