Ayubu 38
38
BWANA amjibu Ayubu
1 #
Kut 19:16,18; 1 Fal 19:11; 2 Fal 2:1; Eze 1:4 Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
2Ni nani huyu atiaye ushauri giza
Kwa maneno yasiyo na maarifa?
3 #
Kut 23:13; 1 Fal 18:46 Basi jifunge viuno kama mwanamume,
Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.
4 #
Zab 104:5
Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?
Haya! Sema, kama una ufahamu.
5Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake – hakika unajua!
Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
6Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?
Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7 #
Ayu 1:6
Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,
Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
8 #
Yer 5:22; Mwa 1:9; Zab 33:7; Mit 8:29 Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango,
Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.#38:8 Katika Kiebrania hakuna mwa nchi.
9Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake,
Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,
10Nikaiagiza amri yangu;
Nikaiwekea makomeo na milango,
11Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita,
Na hapa mawimbi yako yenye nguvu yatazuiliwa?
12Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza?
Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?
13Yapate kuishika miisho ya nchi,
Waovu wakung'utwe wakawe mbali nayo?
14Hubadilika mfano wa udongo chini ya mhuri,
Vitu vyote vinatokea kama mavazi.
15Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie,
Na mkono ulioinuka huvunjika.
16Je! Umeziingia chemchemi za bahari,
Au umetembea mahali pa siri pa vilindi?
17Je! Umefunuliwa malango ya mauti,
Au umeyaona malango ya kuzimu?
18Umeyafahamu mapana ya dunia?
Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.
19Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru?
Na giza pia, mahali pake ni wapi?
20Upate kuipeleka hata mpaka wake,
Upate kuyaelewa mapito ya kuiendea nyumba yake?
21Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo,
Na hesabu ya siku zako ni kubwa!
22Je! Umeziingia ghala za theluji,
Au umeziona ghala za mvua ya mawe,
23 #
Kut 9:18; Yos 10:11; Zab 9:13; Isa 30:30 Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba,
Kwa siku ya mapigano na vita?
24Je! Nuru hutengwa kwa njia gani,
Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?
25Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika,
Au njia kwa umeme wa radi;
26Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu;
Juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu;
27 #
Zab 107:35
Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa,
Na kuyameza majani yaliyo mororo?
28 #
1 Sam 12:17,18; Zab 147:8; Ayu 5:9,10 Je! Mvua ina baba?
Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande?
29 #
Ayu 6:16; Zab 147:16 Barafu ilitoka katika tumbo la nani?
Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa?
30Maji hugandamana kama jiwe,
Na uso wa vilindi huganda kwa baridi.
31 #
Ayu 9:9; Amo 5:8 Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia,
Au kuvilegeza vifungo vya Orioni?
32Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake?
Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?
33 #
Mwa 1:10; Yer 31:35; Zab 119:90,91 Je! Unazijua amri zilizoamriwa mbingu?
Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?
34Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni,
ili wingi wa maji ukufunikize?
35Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda,
Ukakuambia, Sisi tupo hapa?
36 #
Ayu 32:8; Zab 51:6; Mhu 2:26 Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni?
Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?
37Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima?
Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni?
38Wakati mavumbi yagandamanapo,
Na madongoa kushikamana pamoja?
39Je! Utamwindia simba mke mawindo?
Au utashibisha njaa ya simba wachanga,
40Waoteapo mapangoni mwao,
Wakaapo mafichoni wapate kuvizia?
41 #
Zab 147:9; Mt 6:26; Lk 12:24 Ni nani anayempatia kunguru chakula,
Makinda yake wanapomlilia Mungu,
Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?
Iliyochaguliwa sasa
Ayubu 38: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: