Ayubu 40
40
1BWANA akafululiza kumjibu Ayubu, na kusema,
2 #
Ayu 9:3; Isa 45:9 Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi?
Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.
Jibu la Ayubu kwa Mungu
3Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema,
4 #
Ezr 9:6; Zab 51:4; Ayu 29:9; Zab 39:9; Zek 2:13 Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini?
Naweka mkono wangu kinywani pangu.
5Nimenena mara moja, nami sitajibu;
Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.
Mungu amchochea Ayubu
6 #
Ayu 38:1; Zab 50:3 Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
7 #
Ayu 38:3; 42:4 Jifunge viuno kama mwanamume,
Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie.
8 #
Zab 51:4
Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha?
Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?
9 #
Ayu 37:4; Zab 29:3 Au je! Wewe una mkono kama Mungu?
Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?
10 #
Zab 93:1
Haya! Jivike sasa fahari na ukuu;
Jipambe heshima na enzi.
11Mwaga mafuriko ya hasira zako,
Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhalilishe.
12 #
Isa 2:12; Dan 4:37; Lk 18:14 Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe,
Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo.
13Wafiche mavumbini pamoja,
Wafunge nyuso zao mahali palipositirika.
14Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako,
Ya kuwa mkono wako wa kulia waweza kukuokoa.
15Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe;
Yeye hula nyasi kama ng'ombe,
16Tazama basi, nguvu zake zimo katika viuno vyake,
Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.
17Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;
Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.
18Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;
Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.
19Yeye ni wa kwanza kwa hayo matendo makuu ya Mungu;
Ni Muumba wake tu awezaye kumkabili kwa upanga wake.
20 #
Zab 104:14
Hakika milima humtolea chakula;
Hapo wachezapo wanyama pori wote.
21Hulala chini ya miti yenye vivuli,
Mafichoni penye mianzi, na matopeni.
22Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao;
Mierebi ya vijito humzunguka.
23 #
Mwa 13:10; Yer 12:5 Tazama, mto ukifurika, yeye hatetemeki;
Hujiona yu salama, ijapokuwa Yordani hufurika hata kinywani pake.
24Je! Mtu yeyote atamnasa akiwa yu macho,
Au, kumtoboa pua yake kwa mtego?
Iliyochaguliwa sasa
Ayubu 40: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: