Yoshua 1
1
Agizo la Mungu kwa Yoshua
1 #
Kum 1:38
Baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, 2#Kum 34:5 Musa mtumishi wangu amefariki; sasa ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hadi nchi niwapayo wana wa Israeli. 3#Kum 11:24-25 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa. 4#Mwa 15:18; Kut 23:31; Hes 34:3; Kum 1:7; 3:25; 1 Nya 5:9 Toka jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu. 5#Kum 31:6,8; Ebr 13:5; Kum 7:24; Zab 46:11; Rum 8:31,37; Kut 3:12 Hakuna mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha. 6#Kum 31:6,7,23 Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. 7#Hes 27:23; Yos 11:15 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda kulingana na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. 8#Kum 17:18,19; Zab 1:2; 1 Nya 22:13; Mit 3:1 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. 9#Zab 27:1; Yer 1:8 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.
Matayarisho ya kuvuka Mto Yordani
10Ndipo Yoshua akawaamuru viongozi wa watu, akisema, 11#Yos 3:2; Kum 9:1; 11:31 Piteni katika kambi, mkawaamuru hao watu, mkisema, Tayarisheni vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.
12 #
Hes 32:28-32; Kum 3:18-20; Yos 22:1-6 Tena Yoshua akawaambia Wareubeni, na Wagadi, na hao wa nusu ya kabila la Manase, akasema, 13#Hes 32:20; Yos 22:2-4 Likumbukeni neno lile alilowaamuru Musa mtumishi wa BWANA, akisema, BWANA, Mungu wenu, anawapa ninyi raha, naye atawapa nchi hii. 14Wake zenu, na watoto wenu, na makundi yenu, watakaa katika nchi aliyowapa Musa ng'ambo ya Yordani; bali ninyi mtawatangulia ndugu zenu kuvuka, mkiwa mmevaa silaha zenu, watu wote wenye nguvu, na ushujaa, ili mpate kuwasaidia; 15#Yos 22:4 hadi BWANA atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wamepata kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa maawio ya jua. 16Wakamjibu Yoshua, wakasema, Hayo yote uliyotuamuru tutayafanya, na kila mahali utakakotutuma tutakwenda. 17#Mwa 21:22; 26:24,28; 1 Sam 16:18; 20:13; 1 Fal 1:37; Zab 20:1-4,9; Rum 8:31 Kama vile tulivyomsikiliza Musa katika mambo yote, ndivyo tutakavyokusikiliza wewe; BWANA, Mungu wako, na awe pamoja nawe tu, kama alivyokuwa pamoja na Musa. 18Kila mtu atakayeiasi amri yako, asiyasikilize maneno yako katika mambo yote utakayomwamuru, atauawa. Uwe hodari na moyo wa ushujaa, hilo tu.
Iliyochaguliwa sasa
Yoshua 1: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: