Yoshua 20
20
Miji ya makimbilio
1 #
Hes 35:6-32; Kum 4:41-43; 19:1-13 Kisha BWANA akanena na Yoshua, na kumwambia, 2#Kut 21:13; Hes 35:6-14; Kum 4:41-43; 19:2,9; Rum 8:1,33,34; Ebr 6:18,19 Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Haya, toeni hiyo miji ya makimbilio, ambayo niliwaambia habari zake kwa mkono wa Musa; 3ili kwamba mwenye kuua mtu, aliyemwua mtu yeyote pasipo kukusudia, na pasipo kujua, apate kukimbilia huko; nayo itakuwa ni mahali pa kukimbilia kwenu, kumkimbia huyo ajilipizaye kisasi cha damu. 4#Kum 21:19; Rut 4:1,2; Ayu 5:4; Yer 38:7 Naye ataikimbilia miji hiyo mmojawapo, naye atasimama hapo penye maingilio ya lango la huo mji, kisha atanena neno lake masikioni mwa wazee wa mji; nao watamtia kwao ndani ya mji, na kumpa mahali, ili apate kukaa kati yao. 5#Hes 35:12 Na kama huyo mwenye kujilipiza kisasi cha damu akimfuatia, ndipo hawatamtoa huyo mwuaji kumtia mkononi mwake huyo; kwa sababu alimpiga mwenziwe naye hakujua, wala hakumchukia tangu hapo. 6#Hes 35:12,25 Naye atakaa katika mji huo, hadi hapo atakaposimama mbele ya mkutano kuhukumiwa, hadi kifo chake kuhani mkuu mwenye kuwapo siku hizo; ndipo yule mwuaji atarudi, na kuuendea mji wake mwenyewe, na nyumba yake mwenyewe, hadi mji huo alioutoka hapo alipokimbia. 7#Yos 21:32; 1 Nya 6:76; Mwa 33:18,19; Yos 21:21; 2 Nya 10:1; Yos 14:15; 21:11,13; Lk 1:39 Nao wakaweka Kedeshi katika Galilaya katika nchi ya vilima ya Naftali, na Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-arba (ndio Hebroni) katika nchi ya vilima ya Yuda. 8#Kum 4:43; Yos 21:36,38; 1 Nya 6:78; 1 Fal 22:3; Yos 21:27 Tena ng'ambo ya pili ya Yordani pande za Yeriko upande wa kuelekea mashariki wakaweka Bezeri ulioko nyikani, katika nchi tambarare ya kabila la Reubeni, na Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani katika Bashani katika kabila la Manase. 9#Hes 35:15 Miji hiyo ndiyo miji iliyoamriwa kwa ajili ya wana wa Israeli wote, na kwa ajili ya mgeni akaaye kati yao ugenini, ili kwamba mtu yeyote atakayemwua mtu pasipo kukusudia apate kimbilia huko, asife kwa mkono wa mwenye kujilipiza kisasi cha damu, hadi hapo atakapokuwa amekwisha simama mbele ya mkutano.
Iliyochaguliwa sasa
Yoshua 20: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: