Yoshua 21
21
Miji waliyogawiwa Walawi
1 #
Hes 34:17; Yos 14:1; 17:4 Wakati huo hao vichwa vya nyumba za mababa ya Walawi wakamwendea kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni na viongozi wa hao waliokuwa viongozi wa familia za makabila ya Waisraeli; 2#Hes 35:1-8; Yos 18:1; Eze 48:9-18; Mt 10:10; Gal 6:6; 1 Tim 5:17,18 wakanena nao hapo Shilo katika nchi ya Kanaani, wakisema, Yeye BWANA aliamuru kwa mkono wa Musa kwamba sisi tupewe miji tupate kukaa humo, mbuga zake za malisho kwa ajili ya mifugo wetu. 3Basi wana wa Israeli wakawapa Walawi miji hii, pamoja na mbuga zake za malisho, katika urithi wao, sawasawa na hiyo amri ya BWANA.
4 #
Yos 24:33
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni, na katika kabila la Benyamini.
5Kisha Wakohathi wengine waliosalia walipata kwa kura miji kumi katika jamaa za kabila la Efraimu, na katika kabila la Dani, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase.
6Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani.
7Na wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao walipata miji kumi na miwili katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi, na katika kabila la Zabuloni.
8 #
Mwa 49:7; Hes 35:2,3; Yos 18:6; Mit 16:33 Kisha wana wa Israeli waliwapa Walawi kwa kura miji hiyo pamoja na mbuga zake za malisho, kama BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa. 9Kisha wakawapa katika kabila la wana wa Yuda, na katika kabila la wana wa Simeoni, miji hii iliyotajwa hapa kwa majina; 10nayo ilikuwa kwa ajili ya wana wa Haruni, wa jamaa ya Wakohathi, waliokuwa wa wana wa Lawi; kwa kuwa kura ya kwanza ilikuwa ni yao. 11#1 Nya 6:55; Mwa 23:2; Yos 14:15; 15:13; 2 Sam 2:1-3; Lk 1:39 Nao wakawapa Kiriath-arba, ndio Hebroni, (huyo Arba alikuwa baba yake Anaki), katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na mbuga zake za malisho yaliyouzunguka pande zote. 12#Yos 14:14 Lakini mashamba ya mji, na vile vijiji vyake, wakampa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.
13 #
Hes 35:13-15; Yos 20:7-9; 1 Nya 6:57; Yos 15:54; 10:29; 15:42; Isa 37:8 Kisha wakawapa wana wa Haruni, kuhani, Hebroni pamoja na mbuga zake za malisho yake, huo mji wa kukimbilia kwa ajili ya mwuaji, na Libna pamoja na malisho yake; 14#Yos 15:48,50 na Yatiri pamoja na mbuga zake za malisho, na Eshtemoa pamoja na mbuga zake za malisho; 15#1 Nya 6:58; Yos 15:49 na Holoni pamoja na mbuga zake za malisho, na Debiri pamoja na mbuga zake za malisho; 16#1 Nya 6:59; Yos 15:10,55 na Aini, pamoja na mbuga zake za malisho, na Yuta pamoja na mbuga zake za malisho, na Beth-shemeshi pamoja na mbuga zake za malisho; miji tisa katika makabila hayo mawili. 17#Yos 18:24,25 Tena katika kabila la Benyamini, Gibeoni pamoja na mbuga zake za malisho, na Geba pamoja na mbuga zake za malisho; 18#1 Nya 6:60 na Anathothi pamoja na mbuga zake za malisho, na Almoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. 19Miji yote ya wana wa Haruni, makuhani, ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na mbuga zake za malisho.
20 #
1 Nya 6:66
Na jamaa za wana wa Kohathi, Walawi, hao wana wengine wa Kohathi waliosalia, wao walikuwa na miji ya kura yao katika kabila la Efraimu. 21#Mwa 33:19; Yos 20:7; Amu 9:1; 1 Fal 12:1 Nao wakawapa Shekemu pamoja na mbuga zake za malisho, katika nchi ya vilima ya Efraimu, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Gezeri pamoja na mbuga zake za malisho; 22na Kibisaumu pamoja na mbuga zake za malisho, na Beth-horoni pamoja na mbuza zake za malisho, miji minne. 23Tena katika kabila la Dani Elteke pamoja na mbuga zake za malisho, na Gibethoni pamoja na mbuga zake za malisho; 24na Aiyaloni pamoja na mbuga zake za malisho, na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. 25Tena katika hiyo nusu ya kabila la Manase, Taanaki pamoja na mbuga zake za malisho, na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji miwili. 26Miji yote ya jamaa za wana wa Kohathi waliosalia ilikuwa ni miji kumi, pamoja na mbuga zake za malisho.
27 #
1 Nya 6:71; Kum 1:4; 4:43; Yos 20:8; 1 Nya 6:71,76 Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na mbuga zake za malisho; miji miwili. 28Tena katika kabila la Isakari, Kishioni pamoja na malisho yake, na Daberathi pamoja na mbuga zake za malisho; 29na Yarmuthi pamoja na mbuga zake za malisho, na Enganimu pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. 30Tena katika kabila la Asheri, Mishali pamoja na mbuga zake za malisho, na Abdoni pamoja na mbuga zake za malisho; 31na Helkathi pamoja na mbuga zake za malisho, na Rehobu pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. 32#Yos 20:7 Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu. 33Miji yote ya Wagershoni kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na mbuga zake za malisho.
34 #
1 Nya 6:77
Tena jamaa za wana wa Merari, hao Walawi waliosalia, katika kabila la Zabuloni, Yokneamu pamoja na mbuga zake za malisho, na Karta pamoja na mbuga zake za malisho, 35na Dimna pamoja na mbuga zake za malisho, na Nahalali pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. 36Tena katika kabila la Reubeni, Bezeri pamoja na mbuga zake za malisho, na Yahasa pamoja na mbuga zake za malisho, 37na Kedemothi pamoja na mbuga zake za malisho, na Mefaathi pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. 38#Kum 4:43; 1 Fal 4:13; Mwa 32:1; 2 Sam 2:8; 17:27 Tena katika kabila la Gadi Ramothi katika Gileadi pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Mahanaimu pamoja na mbuga zake za malisho; 39na Heshboni pamoja na mbuga zake za malisho, na Yazeri pamoja na mbuga zake za malisho; jumla yake miji minne. 40Miji hiyo yote ilikuwa ni miji ya wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao, ni hizo jamaa za Walawi zilizosalia; na kura yao ilikuwa ni miji kumi na miwili.
41 #
Mwa 49:7; Hes 35:7; Kum 33:10 Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arubaini na minane, pamoja na mbuga zake za malisho. 42Miji hiyo kila mmoja ulikuwa pamoja na mbuga zake za malisho, yaliyouzunguka pande zote; ndivyo ilivyokuwa katika miji hiyo yote.
43 #
Mwa 13:15; 15:18; 26:3 Basi BWANA aliwapa Israeli nchi hiyo yote, ambayo aliapa kwamba atawapa baba zao; nao wakaimiliki, na kukaa humo. 44#Yos 11:23; 22:4; Kum 7:24 Kisha BWANA akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao. 45#Yos 23:14; Kut 3:7,8; 23:23,31; 1 Fal 8:56; Isa 49:7,8,15,16; Mt 24:35; Lk 21:33 Halikuanguka neno lolote katika jambo lolote lililokuwa ni jema ambalo BWANA alikuwa amelinena katika habari ya nyumba ya Israeli; yalitimia mambo yote.
Iliyochaguliwa sasa
Yoshua 21: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.