Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo ya Walawi 12

12
Utakaso wa wanawake baada ya kujifungua
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Lk 2:22; Law 15:19 Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto wa kiume, ndipo atakuwa najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi ndivyo atakavyokuwa najisi. 3#Mwa 17:12; Lk 1:59; 2:21; Yn 7:22,23 Siku ya nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake. 4Na huyo mwanamke atakaa muda wa siku thelathini na tatu ili kutakata damu yake. 5Lakini kama amezaa mtoto wa kike naye atakaa muda wa siku sitini na sita ili kutakata damu yake. 6#Lk 2:22; Isa 53:7; Lk 24:26,27; Yn 1:29,36; 1 Pet 1:18,19; Ufu 5:6-8; 7:14 Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mtoto wa kiume, au kwa ajili ya mtoto wa kike ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani; 7#Ebr 9:9-28; 10:1-12 na yeye atawasongeza mbele za BWANA, na kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atatakasika. Hii ndiyo amri yake huyo azaaye, awe ni mtoto wa kiume au wa kike. 8#Lk 2:24; Law 5:7; 2 Kor 8:9; Law 4:26 Kama mali yake huyo mwanamke haimudu mwana-kondoo, hapo ndipo atakapochukua hua wawili, au makinda mawili ya njiwa; mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na wa pili kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.

Iliyochaguliwa sasa

Mambo ya Walawi 12: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia