Mathayo 7
7
Kuwahukumu wengine
1 #
Rum 2:1; 1 Kor 4:5 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. 2#Mk 4:24 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 3Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huioni? 4Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Kutweza kitakatifu
6 #
Mt 10:11
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Omba, tafuta, bisha
7 #
Mk 11:24; Lk 11:9-13; Yer 29:13,14; Yn 14:13; 16:23 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. 9Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? 10Au akiomba samaki, atampa nyoka? 11#Yak 1:17 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?
Amri kuu
12 #
Lk 6:31; Mt 22:39,40; Rum 13:8-10 Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.
Mlango mwembamba
13 #
Lk 13:24; Yn 10:7,9 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14#Mt 19:24; Mdo 14:22 Bali mlango ni mwembamba, na njia imebana iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Mti na matunda yake
15 #
Mt 24:4,5,24; Mdo 20:29 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. 16#Gal 5:19-22; Yak 3:12 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17#Mt 12:33 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19#Mt 3:10; Lk 3:9; Yn 15:2,6 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20#Mt 12:33 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
Kuhusu wanaojihadaa
21 #
Mt 21:29; Rum 2:13; Yak 1:22,25; 2:14; 1 Kor 12:3 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22#Yer 14:14; 27:15; Lk 13:25-27; 1 Kor 13:1,2 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23#Zab 6:9; Mt 13:41; 25:41; 2 Tim 2:19 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Wasikiao na watendao
24 #
Mt 7:21
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27#Eze 13:10,11 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
28 #
Mk 1:22; Lk 4:32; Mt 11:1; 13:53; 19:1; 26:1 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29#Yn 7:46 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao.
Iliyochaguliwa sasa
Mathayo 7: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: