Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nehemia 6

6
Kushindwa kwa adui
1 # Neh 2:10; 3:1-3 Basi ikawa, walipoarifiwa Sanbalati, na Tobia, na Geshemu, Mwarabu na adui zetu hao wengine, kwamba nimeujenga ukuta, wala hayakubakia mapengo ndani yake; (ijapokuwa hata wakati ule sijaisimamisha milango katika malango); 2#Mit 26:24; 1 Nya 8:12; Neh 11:25,35; Zab 12:2; Mit 26:24; Mhu 4:4; Mik 7:4,5 Sanbalati na Geshemu wakatuma wajumbe kwangu, wakasema, Njoo, tukutane huko vijijini katika nchi tambarare ya Ono. Lakini wakakusudia kunifanyia mabaya. 3#Mit 14:15 Na mimi nikatuma wajumbe kwao, nikasema, Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi, siwezi kushuka, kwa nini niwashukie na hapo kazi isimame? 4#Mit 1:10 Nao wakaniletea mwito huo mara nne; nikawajibu maneno yale yale. 5Ndipo Sanbalati akamtuma kwangu mtumishi wake vile vile mara ya tano, na barua wazi mkononi mwake; 6#Yer 9:3; Rum 3:8; 2 Kor 6:8; 1 Pet 2:12; Neh 2:19; Ezr 4:13; Lk 23:2 nayo yakaandikwa humo, Habari imeenea katika mataifa, naye Geshemu asema neno lilo hilo, ya kwamba wewe na Wayahudi mnakusudia kuasi; ndiyo sababu unaujenga huo ukuta; nawe unataka kuwamiliki, ndivyo wasemavyo. 7Nawe umewaweka manabii ili wakuhubirie huko Yerusalemu kwa kusema, Yuko mfalme katika Yuda; basi sasa mfalme ataarifiwa mambo haya, Basi sasa, njoo ili tushauriane. 8#Ayu 13:4; Zab 36:3; Isa 59:4; Dan 11:27 Ndipo mimi nikatuma kwake wajumbe, kusema, Hakukufanyika mambo kama hayo uyasemayo, lakini kwa moyo wako wewe mwenyewe umeyabuni. 9#Kum 33:25; Zab 56:3; Isa 41:10; 2 Kor 12:9 Kwani hao wote walitaka kutuogofya, wakisema, Kwa kuwa mikono yao italegea katika kazi, kazi isifanyike. Lakini sasa Ee Mungu, itie nguvu mikono yangu.
10 # Mit 26:24 Nikaingia nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyekuwa amefungwa kifungo cha nyumbani; naye akasema, Tukutane nyumbani mwa Mungu, ndani ya hekalu, na tuifunge milango ya hekalu; kwa kuwa watakuja kukuua; naam, wakati wa usiku watakuja kukuua. 11#Mit 28:1 Nami nikasema, Je! Mtu kama mimi nikimbie? Naye ni nani, akiwa kama nilivyo mimi, atakayeingia hekaluni ili kuponya maisha yake? Sitaingia. 12#Eze 13:22 Nikatambua, na tazama, si Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; kwa kuwa Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri. 13Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie. 14#Neh 13:29; Eze 13:17 Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati kulingana na hayo matendo yao, na yule nabii mwanamke Noadia.#6:14 Noadia maana yake yule ambaye BWANA hukutana naye (Ezr 8:33), na hao manabii waliosalia, waliotaka kuniogofya.
Ukuta wakamilika
15Basi huo ukuta ukakamilika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili. 16#Neh 2:10; 4:1; 6:1; Zab 126:2 Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo wamataifa wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu. 17Tena siku zile wakuu wa Yuda walimtumia nyaraka nyingi Tobia nazo nyaraka za Tobia ziliwafikia. 18Kwa maana walikuwa watu wengi katika Yuda waliomwapia, kwa sababu alikuwa mkwewe Shekania, mwana wa Ara; naye Yehohanani mwanawe amemwoa binti Meshulamu, mwana wa Berekia. 19Tena waliyanena mema yake mbele yangu, na kumwambia maneno yangu. Tobia naye akaniletea mimi nyaraka za kuniogofya.

Iliyochaguliwa sasa

Nehemia 6: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia