Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 33

33
Vituo vya safari ya Waisraeli wakitoka Misri
1Hivi ndivyo vituo vya wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni. 2Musa akaandika jinsi walivyotoka katika vituo, kituo baada ya kituo kwa kufuata amri ya BWANA; na hivi ndivyo vituo: 3#Mwa 47:11; Kut 1:11; 12:37; 12:2; 13:4; Zab 105:38; Isa 52:12; Kut 14:8 Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa uhodari mkubwa mbele ya macho ya Wamisri wote, 4#Kut 12:12; 18:11; Isa 19:1; Sef 2:11; Ufu 12:8 hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo.
5 # Kut 12:37 Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapiga kambi katika Sukothi. 6#Mwa 33:17; Kut 13:20; Yos 13:27; Zab 60:6 Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika. 7#Kut 13:17,18; 14:2,9 Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapiga kambi mbele ya Migdoli. 8#Kut 14:22; 15:22 Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapiga kambi Mara. 9Wakasafiri kutoka Mara, wakafika Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapiga kambi Elimu. 10Wakasafiri kutoka Elimu wakapiga kambi karibu na Bahari ya Shamu. 11#Kut 16:1; 17:1 Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapiga kambi katika nyika ya Sini. 12Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapiga kambi Dofka. 13Wakasafiri kutoka Dofka, wakapiga kambi Alushi. 14#Kut 17:1; 19:2 Wakasafiri kutoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa. 15#Kut 16:1; 19:1,2 Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapiga kambi katika nyika ya Sinai. 16#Hes 11:34; Kum 9:22 Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapiga kambi Kibroth-hataava. 17Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapiga kambi Haserothi. 18#Hes 12:16; Kum 1:1 Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapiga kambi Rithma. 19Wakasafiri kutoka Rithma, wakapiga kambi Rimon-peresi. 20#Kum 1:1 Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapiga kambi Libna. 21Wakasafiri kutoka Libna, wakapiga kambi Risa. 22Wakasafiri kutoka Risa, wakapiga kambi Keheletha. 23Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapiga kambi katika mlima wa Sheferi 24Wakasafiri kutoka huo mlima wa Sheferi, wakapiga kambi Harada. 25Wakasafiri kutoka Harada, wakapiga kambi Makelothi. 26Wakasafiri kutoka Makelothi, wakapiga kambi Tahathi. 27Wakasafiri kutoka Tahathi wakapiga kambi Tera. 28Wakasafiri kutoka Tera, wakapiga kambi Mithka. 29Wakasafiri kutoka Mithka, wakapiga kambi Hashmona. 30#Kum 10:6 Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapiga kambi Moserothi. 31Wakasafiri kutoka Moserothi, wakapiga kambi Bene-yaakani. 32#Mwa 36:27; Kum 10:6; 1 Nya 1:42 Wakasafiri kutoka Bene-yaakani, wakapiga kambi Hor-hagidgadi. 33Wakasafiri kutoka Hor-hagidgadi, wakapiga kambi Yotbatha. 34Wakasafiri kutoka Yotbatha, wakapiga kambi Abrona. 35#Kum 2:8; 1 Fal 9:26; 22:48 Wakasafiri kutoka Abrona, wakapiga kambi Esion-geberi. 36#Hes 13:21; 20:1; Kum 32:51; Yos 15:1 Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapiga kambi katika nyika ya Sini (ni Kadeshi). 37#Hes 20:22,23; 21:4; Eze 47:19 Wakasafiri kutoka Kadeshi wakapiga kambi katika mlima wa Hori, katika mpaka wa nchi ya Edomu, 38#Hes 20:22-28; Kum 10:6; 32:50 Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya BWANA, akafa hapo, katika mwaka wa arubaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi. 39Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia moja ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori. 40#Hes 21:1; Amu 1:16 Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli. 41Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapiga kambi Salmona. 42Wakasafiri kutoka Salmona, wakapiga kambi Punoni. 43Wakasafiri kutoka Punoni, wakapiga kambi Obothi. 44Wakasafiri kutoka Obothi, wakapiga kambi Lye-abarimu, katika mpaka wa Moabu. 45#Hes 32:34 Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapiga kambi Dibon-gadi. 46#Yer 48:22; Eze 6:14 Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapiga kambi Almon-diblathaimu. 47#Hes 21:20; Kum 32:49 Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapiga kambi katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo. 48#Hes 22:1 Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapiga kambi katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko. 49Wakapiga kambi karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu.
Maagizo ya kuishinda Kanaani
50Kisha BWANA akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia, 51#Kum 7:1; 9:1; Yos 3:17 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, 52#Kut 23:24; 34:12-17; Kum 7:2-5,25,26; Yos 11:12; 23:7; Amu 2:2 ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunjavunja mahali pao pote palipoinuka; 53#Zab 24:1; Kum 10:14; Ayu 41:11; Dan 4:35 nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuishi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki. 54#Hes 26:54-56 Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama makabila ya baba zenu yalivyo. 55#Yos 23:13; Zab 106:34; Kut 23:33; Eze 28:24 Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtawabakiza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa. 56Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 33: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia