Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 20

20
1 # Mwa 9:21; Isa 28:7 Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi;
Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.
2Utisho wa mfalme ni kama ngurumo ya simba;
Amkasirishaye huitendea dhambi nafsi yake.
3 # Mwa 13:7 Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake;
Bali kila mpumbavu ataka kugombana.
4Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi;
Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.
5Mashauri ya moyoni ni kama kilindi;
Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka.
6 # Mt 6:2; Zab 12:1; Mhu 7:28; Yer 5:1; Lk 18:8 Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe;
Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
7Mwenye haki aendaye katika unyofu wake,
Watoto wake wabarikiwa baada yake.
8Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu,
Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake.
9 # Ayu 14:4; Mhu 7:20; 1 Yoh 1:8 Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu;
Nimetakasika dhambi yangu?
10Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali,
Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA.
11 # Mt 7:16 Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake;
Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.
12 # Kut 4:11; Rum 11:36 Sikio lisikialo, na jicho lionalo,
BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.
13 # Rum 12:11 Usipende usingizi usije ukawa maskini;
Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.
14Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi;
Lakini akiisha kwenda zake hujisifu.
15Dhahabu iko, na marijani tele;
Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani.
16Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni;
Mtoze rehani aliye mdhamini wa wageni.
17Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu;
Lakini halafu kinywa chake kitajaa changarawe.
18Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana;
Na kwa shauri la akili fanya vita.
19Mwenye udaku hufunua siri;
Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.
20 # Kut 21:17; Law 20:9; Mt 15:4; Rum 3:23 Amlaaniye babaye au mamaye,
Taa yake itazimika katika giza kuu.
21 # Mit 28:8; Hab 2:6 Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka,
Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.
22 # Kum 32:35; Rum 12:17; 1 Pet 3:9 Usiseme, Mimi nitalipa mabaya;
Mngojee BWANA, naye atakuokoa.
23Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa BWANA;
Tena mizani ya hila si njema.
24 # Yer 10:23; Rum 8:26 Mwenendo wa mtu watoka kwa BWANA;
Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake?
25Ni mtego, mtu aseme kwa haraka, Kitu hiki ni wakfu;
Na baada ya kuweka nadhiri kuulizauliza habari.
26Mfalme mwenye hekima huwapepeta wasio haki;
Naye hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.
27Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA;
Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.
28Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme,
Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili.
29Fahari ya vijana ni nguvu zao,
Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.
30Machubuko ya fimbo husafisha uovu,
Na mapigo hufikia ndani ya mtima.

Iliyochaguliwa sasa

Mithali 20: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia