Zaburi 109
109
Sala ya uthibitisho na kutaka kisasi
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi. Zaburi.
1 #
Zab 83:1
Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,
2Kwa maana vinywa viovu na vyenye hila vimefumbuliwa juu yangu,
Vikinisema kwa ulimi wa uongo,
Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
3 #
1 Sam 19:4,5; Zab 35:7,20; Yn 15:25 Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka,
Wamepigana nami bure.
4Badala ya upendo wangu wao hunishitaki,
Ijapokuwa niliwaombea.
5 #
Zab 38:20
Wamenilipa mabaya kwa mema yangu,
Na chuki badala ya upendo wangu.
6Umweke mtu mkorofi juu yake,
Mshitaki na asimame kulia kwake.
7 #
Mit 28:9
Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki,
Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.
8 #
Mdo 1:20
Siku zake na ziwe chache,
Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.
9 #
Kut 22:24; Yer 18:21 Wanawe na wawe yatima,
Na mkewe na awe mjane.
10 #
Mwa 4:12
Kutanga na watange wanawe na kuomba,
Watafute chakula mbali na mahame yao.
11 #
Ayu 18:9
Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo,
Wageni na wateke mapato ya kazi yake.
12Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili,
Wala mtu wa kuwahurumia yatima wake.
13 #
Zab 37:28; Mit 10:7 Wazawa wake waangamizwe,
Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.
14 #
Kut 20:5; Neh 4:5 Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za BWANA,
Na dhambi ya mamaye isifutwe.
15 #
Ayu 18:17
Ziwe mbele za BWANA daima,
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
16Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili,
Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,
Hata akamwua mtu aliyevunjika moyo,
17Naye alipenda kulaani, nako kukampata.
Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,
18Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake.
Ikamwingilia moyoni kama maji,
Na kama mafuta mifupani mwake.
19Na iwe kwake kama vazi ajivikalo,
Na kama mshipi ajifungao daima.
20Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa BWANA,
Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.
21Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako,
Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.
22Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji,
Na moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
23Ninapita kama kivuli kianzacho kutoweka,
Ninapeperushwa kama nzige.
24 #
Ebr 12:12
Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga,
Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.
25 #
Isa 37:22; Mt 27:39; Mk 15:29 Nami nimekuwa wa kudharauliwa na watu,
Wanionapo hutikisa vichwa vyao.
26Ee BWANA, Mungu wangu, unisaidie,
Uniokoe kulingana na fadhili zako.
27 #
Ayu 37:7
Nao wakajue ya kuwa huu ni mkono wako;
Wewe, BWANA, umeyafanya hayo.
28 #
Hes 22:12; Isa 65:14 Waache walaani, bali Wewe utabariki,
Wanaonishambulia na waaibishwe,
Naye mtumishi wako afurahi.
29Washitaki wangu watavikwa fedheha,
Na wavikwe aibu yao kama joho.
30Nitamshukuru BWANA kwa kinywa changu,
Naam, nitamsifu katikati ya mkutano.
31Maana atasimama mkono wa kulia wa mhitaji
Amwokoe kutoka kwa wanaoihukumu nafsi yake.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 109: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: