Zaburi 111
111
Sifa kwa maajabu ya Mungu
1Haleluya.#111:1 Haleluya: maana yake ni, Msifuni BWANA.
Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
2 #
Ayu 38:1
Matendo ya BWANA ni makuu,
Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.
3Kazi yake imejaa heshima na adhama,
Na haki yake yadumu milele.
4Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;
BWANA ni mwenye fadhili na rehema.
5Amewapa wamchao chakula;
Atalikumbuka agano lake milele.
6Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake,
Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
7 #
Zab 19:7
Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,
Maagizo yake yote ni amini,
8 #
Ufu 15:3
Yamethibitika milele na milele,
Yamefanywa kwa uaminifu na haki.
9 #
Ufu 15:3
Amewapelekea watu wake ukombozi,
Ameamuru agano lake liwe la milele,
Jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
10 #
Kum 4:6; Ayu 28:28; Mit 1:7; 9:10; Mhu 12:3 Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima,
Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri,
Sifa zake zadumu milele.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 111: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: