Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 16:7-11

Zaburi 16:7-11 SRUV

Nitamhimidi BWANA aniongozaye, Wakati wa usiku pia moyo wangu hunishauri. Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa. Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini. Maana hutaitupa kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu. Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.

Soma Zaburi 16