Zaburi 24:7-10
Zaburi 24:7-10 SRUV
Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani Mfalme wa utukufu? BWANA mwenye nguvu, hodari, BWANA hodari wa vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.