Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 76

76
Mungu wa Waisraeli – Mungu mkuu
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1Katika Yuda Mungu amejulikana,
Katika Israeli jina lake ni kuu.
2Kibanda chake pia kiko Salemu,
Na maskani yake iko Sayuni.
3 # Zab 46:9; Eze 39:9 Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta,
Ngao, upanga, na zana za vita.
4 # Eze 38:12 Wewe U mwenye fahari na adhama,
Toka milima ya mateka.
5 # Isa 46:12; Zab 13:3; Yer 51:39 Wametekwa wenye moyo thabiti;
Wamelala usingizi;
Wala hawakuiona mikono yao
Watu wote walio hodari.
6 # Kut 15:1; Nah 2:13; Zek 12:4 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,
Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.
7 # Ayu 41:10; Nah 1:6 Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe;
Naye ni nani awezaye kusimama ukasirikapo?
8Toka mbinguni ulitangaza hukumu;
Nchi iliogopa, ikakaa kimya.
9Mungu aliposimama ili kuhukumu
Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia.
10 # Kut 9:16 Maana hasira ya binadamu itakusifu,
Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
11 # Mhu 5:4; Zab 68:29 Wekeni nadhiri na mziondoe
Kwa BWANA, Mungu wenu.
Wote wanaomzunguka wamletee hedaya,
Yeye astahiliye kuogopwa.
12 # Zab 68:35 Yeye huzikata roho za wakuu;
Na kuwatisha wafalme wa dunia.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 76: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia