Ufunuo 22
22
Mto wa maji ya uzima
1 #
Eze 47:1; Zek 14:8 Kisha akanionesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo, 2#Mwa 2:9; Eze 47:12; Ufu 21:21 katikati ya njia yake kuu. Na upande huu na huu kando ya ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 3#Zek 14:11 Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumishi wake watamtumikia; 4#Mt 5:8; Ufu 3:12 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5#Isa 60:19; Dan 7:18,27; Ufu 21:25 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
6 #
Ufu 1:1; 1 Kor 14:32 Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi. 7#Ufu 3:11; 1:3 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
Hitimisho na baraka
8 #
Ufu 19:10
Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nilianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionesha hayo. 9Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.
10 #
Ufu 10:4; 1:3; Dan 8:26; 12:4 Akaniambia, Usiyatie mhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. 11#Dan 12:10 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. 12#Isa 40:10; 62:11; Zab 28:4; 62:12; Yer 17:10; Ufu 3:11; Rum 2:6 Tazama, naja upesi, na malipo yangu yako pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13#Ufu 1:8,17; 2:8; Isa 44:6; 48:12; Ebr 13:8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14#Mwa 2:9; 3:22; 49:11 Heri wazifuao nguo zao, ili wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. 15#Ufu 21:8,27; 1 Kor 6:9,10 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
16 #
Isa 11:1,2,10; 5:5; Isa 11:1,10; Lk 1:78; Ufu 1:1,2; 5:5 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzawa wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.
17 #
Isa 55:1; Ufu 21:6; Zek 14:8; Rum 8:23; Yn 7:37 Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.
18 #
Kum 4:2; 12:32; 29:20; Ufu 15:1,6 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19#Mwa 2:9; 3:22 Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
20Yeye ayashuhudiaye haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.
21Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.
Iliyochaguliwa sasa
Ufunuo 22: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: