Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 14:10-15

Zekaria 14:10-15 SRUV

Nchi yote itageuzwa kuwa kama Araba, toka Geba mpaka Rimoni upande wa kusini wa Yerusalemu; naye atainuliwa juu, atakaa mahali pake mwenyewe, toka lango la Benyamini mpaka mahali pa lango la kwanza, mpaka lango la pembeni; tena toka mnara wa Hananeli mpaka mashinikizo ya mfalme. Na watu watakaa ndani yake, wala hakutakuwako laana tena; lakini Yerusalemu utakaa salama. Na hii ndiyo tauni, ambayo BWANA atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu; nyama ya mwili wao itaharibika, wakiwa wamesimama kwa miguu yao, na macho yao yataharibika ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitaharibika vinywani mwao. Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba mashaka makubwa yatokayo kwa BWANA yatakuwa kati yao; na kila mmoja wao atakamata mkono wa jirani yake, na mkono wake utainuliwa ili kushindana na mkono wa jirani yake. Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa pande zote utakusanywa, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana. Na hivyo ndivyo itakavyokuwa tauni ya farasi, na nyumbu, na ngamia, na punda, na ya hao wanyama wote watakaokuwamo kambini mle, kama tauni hiyo.

Soma Zekaria 14

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zekaria 14:10-15