Mwanzo 49:24-25
Mwanzo 49:24-25 BHNTLK
Lakini upinde wake bado imara, na mikono yake imepewa nguvu, kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli; kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.