Mwanzo 49
49
Yakobo anawabariki wanawe#49:1-28 Utenzi huu ambao hapa umepewa kichwa “Yakobo anawabariki wanawe” una orodha ya matamshi ya namna ya majaliwa kwa kila kabila la Israeli, na matamshi yenyewe yanatumia picha au mifano ya wanyama (rejea k.m. aya 9:14,17,21,27). Kama vile Isaka alivyotamka majaliwa ya Yakobo na Esau kabla ya kufariki (Mwa 27:4) vivyo hivyo Yakobo naye anaangalia siku za usoni za wanawe na kutoa uaguzi wake juu yao (rejea Kumb 33; Amu 5:14-18; 2Sam 23:1-7).
1Yakobo akawaita wanawe, akasema, “Kusanyikeni pamoja niwaambieni mambo yatakayowapata siku zijazo.
2“Kusanyikeni msikie, enyi wana wa Yakobo,
nisikilizeni mimi Israeli, baba yenu.
3“Wewe Reubeni#49:3-4 Reubeni: Huyu alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. Lakini alipokonywa haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa kosa lake lililoathiri maadili ya jamii, yaani kwa kulala na Bilha ambaye alikuwa suria wa baba yake (Mwa 35:22; rejea 29:29). ni mzaliwa wangu wa kwanza,
nguvu yangu na tunda la ujana wangu.
Wewe wawapita ndugu zako kwa ukuu na nguvu.
4Wewe ni kama maji ya mafuriko.
Lakini hutakuwa wa kwanza tena,
maana ulipanda kitandani mwangu mimi baba yako,
wewe ulikitia najisi;
naam wewe ulikipanda!
5“Simeoni na Lawi ni ndugu:
silaha zao wanatumia kufanya ukatili,
6lakini mimi sitashiriki njama zao;
ee roho yangu, usishiriki mikutano yao,
maana, katika hasira yao, walimuua mtu,
kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.
7Nalaani hasira yao maana ni kali mno,
na ghadhabu yao isiyo na huruma.
Nitawatawanya katika nchi ya Yakobo,
nitawasambaza katika nchi ya Israeli.
8“Wewe Yuda, ndugu zako watakusifu.
Adui zako utawakaba shingo;
na ndugu zako watainama mbele yako.
9Wewe Yuda, mwanangu, ni kama mwanasimba
ambaye amepata mawindo yake akapanda juu.
Kama simba hujinyosha na kulala chini;
simba mwenye nguvu, nani athubutuye kumwamsha?
10Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda,
wala bakora ya utawala miguuni pake,#49:10 Wala bakora ya utawala miguuni pake: Tafsiri nyingine yamkini: “wazawa wake watatawala daima”.
mpaka atakapofika yule ambaye ni yake;#49:10 Atakapofika yule ambaye ni yake: Tafsiri yamkini ya makala ngumu ya Kiebrania. Pengine maneno haya yamefafanuliwa kwa maana ya kwamba baada ya utawala wa Yuda kudumu kwa muda mrefu usiojulikana, kutatokea mtawala wa kimasiha ambaye watu wa mataifa yote watamtii (Hes 24:17).
ambaye mataifa yatamtii.
11Atafunga punda wake katika mzabibu
na mwanapunda wake kwenye mzabibu bora.
Hufua nguo zake katika divai,
na mavazi yake katika divai nyekundu.#49:11 Aya hii inaeleza hali ya rutuba nyingi ya udongo na kutokana na hali hiyo nchi ina matunda kwa wingi.
12Macho yake ni mekundu kwa divai,
meno yake ni meupe kwa maziwa.#49:12 Macho yake …maziwa: Au: Macho yake ni meusi kuliko divai, meno yake ni meupe kuliko maziwa. Picha ya hali ya juu ya rutuba inaendelea.
13“Zebuluni ataishi sehemu za pwani,#49:13 Zebuluni ataishi sehemu za pwani: Kabila la Zabuloni litafanya biashara ya baharini (Kumb 33:18-19).
pwani yake itakuwa mahali pa kuegesha meli.
Nchi yake itapakana na Sidoni.#49:13 Sidoni: Mji wa Foinike, pwani ya bahari ya Mediteranea, kaskazini ya Palestina. Taz Yos 11:8 maelezo.
14“Isakari ni kama punda mwenye nguvu,
ajilazaye kati ya mizigo yake.
15Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema,
na kwamba nchi ni ya kupendeza,
akauinamisha mgongo wake#49:15 Akauinamisha mgongo wake: Kabila la Isakari litakuwa radhi kutawaliwa na Wakanaani. kubeba mzigo,
akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti.
16“Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake,
kama mojawapo ya makabila ya Israeli.
17Atakuwa kama nyoka njiani,
nyoka mwenye sumu kando ya njia,
aumaye visigino vya farasi,
naye mpandafarasi huanguka chali.
18“Ee Mwenyezi-Mungu, nangojea uniokoe!
19“Gadi atashambuliwa na wanyang'anyi,
lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia.
20“Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi,
naye atatoa chakula kimfaacho mfalme.
21“Naftali ni kama paa aliye huru,
azaaye watoto walio wazuri.
22“Yosefu ni kama mti uzaao,
mti uzaao kando ya chemchemi,
matawi yake hutanda ukutani.
23Wapiga mishale walimshambulia vikali,
wakamtupia mishale na kumsumbua sana.
24Lakini upinde wake bado imara,
na mikono yake imepewa nguvu,
kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,
kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli;
25kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia,
kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki;
upate baraka za mvua toka juu mbinguni,
baraka za maji ya vilindi vilivyo chini,
baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.
26Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele,
ziwe bora kuliko vilima vya kale.
Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake.#49:22-26 Rejea Kumb 33:13-17. Kipande hiki cha utenzi kinatoa kisa cha umaarufu waliokuwa nao wazawa wa Yosefu: makabila ya Efraimu na Manase (Taz Mwa 48:5) ambayo yalimiliki maeneo yenye rutuba sana katika milima ya Palestina ya kati na sehemu ya Mashariki ya Mto Yordani (rejea Hes 32:33,39-42; Yos 16—17).
27“Benyamini#49:27 Benyamini: Kabila la Benyamini lilikuwa kabila dogo kuliko makabila mengine. Lakini umaarufu wake ulijitokeza kutokana na wapiganaji wake hodari (rejea Amu 3:15; 5:14; 20:15-16). Mfalme Sauli alitoka katika kabila hili (rejea 1Sam 9:1-2,21; 10:1-2). Taz pia Rom 11:1; Fil 3:5. ni mbwamwitu mkali;
asubuhi hula mawindo yake,
na jioni hugawa nyara.”
28Hayo ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hayo ndiyo maneno aliyowaambia baba yao alipowabariki, kila mmoja wao kama alivyostahili.#49:28—50:14 Sehemu hii ifuatayo inamalizia na kukamilisha historia ya Yosefu ambayo ilianza katika Mwa 37.
Kifo cha Yakobo
29Kisha Israeli akawaagiza wanawe hivi, “Mimi karibu nife na kujiunga na watu wangu. Nizikeni pamoja na wazee wangu katika pango lililoko shambani mwa Efroni Mhiti, 30kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia. 31Huko ndiko walikozikwa Abrahamu na mkewe Sara; huko ndiko walikozikwa Isaka na mkewe Rebeka; na huko ndiko nilikomzika Lea. 32Shamba hilo na pango lake lilinunuliwa kwa Wahiti.”
33Yakobo alipomaliza kuwausia wanawe, aliirudisha miguu yake kitandani, akatoa roho akajiunga na wazee wake.
Iliyochaguliwa sasa
Mwanzo 49: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993

: