Mwanzo 9
9
Mungu anafanya agano na Noa
1Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni, muongezeke, mkaijaze nchi.#9:1 Noa, kama baba wa kundi jipya la binadamu waliookolewa kutoka gharika kuu, anapewa baraka inayofanana na ile ya Mwa 1:22,28. 2Wanyama wote, ndege wote wa angani, viumbe wote watambaao juu ya nchi na samaki wote wa baharini watakuwa na hofu na kuwaogopa nyinyi. Wote wamewekwa chini ya mamlaka yenu. 3Wanyama wote hai watakuwa chakula chenu kama vile nilivyowapa mimea kuwa chakula chenu. 4Lakini msile nyama yenye damu, kwani uhai uko katika damu.#9:4 Waisraeli wa kale walifikiri kwamba damu ilikuwa chanzo muhimu cha uhai wa wanyama na binadamu. Hivyo, kukatazwa kula nyama yenye damu ilikuwa namna moja ya kusisitiza kwamba uhai ni mali yake Mungu peke yake ambaye ndiye asili na mpaji wa uhai. Rejea Lawi 7:26-27; 17:10-14; 19:26; Kumb 12:23. Mwanzoni mwa Kanisa, Wakristo waliokuwa Wayahudi bado walishika agizo hilo kwa makini (rejea Mate 15:19-20). 5Damu ya uhai wenu nitaidai; nitaidai kutoka kwa kila mnyama na binadamu. Atakayemuua binadamu mwenzake, nitamdai uhai wake.
6Amwagaye damu ya binadamu,
damu yake itamwagwa na binadamu;
maana binadamu aliumbwa#9:6 Kwa mfano wa Mungu, binadamu aliumbwa: Mwa 1:27. Thibitisho hili ya kwamba Mungu aliumba binadamu wote kwa mfano wake linaonesha jinsi ilivyo vibaya mno mauaji ya binadamu hata katika vita. kwa mfano wa Mungu.
7Nanyi zaeni, mkaongezeke;
zaeni kwa wingi, mkaongezeke nchini.”
Upinde wa mvua
8Kisha Mungu akamwambia Noa na wanawe, 9“Ninaweka agano langu nanyi na wazawa wenu 10na viumbe vyote hai: ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wa porini, wote waliotoka katika safina pamoja nanyi. 11Nathibitisha agano langu nanyi, kwamba, kamwe viumbe vyote hai havitaangamizwa kwa gharika, wala haitatokea tena gharika kuiharibu nchi.”#9:8-11 Agano hili linahusu ulimwengu wote. Ndiyo maana ukumbusho wa agano hilo (upinde wa mvua) unawekwa angani. Na agano hilo ni agano la kudumu na halitabatilishwa (aya 11-12). Yahusu ahadi ambayo Mungu anafanya peke yake na sio kwa kupatana na binadamu au Noa. 12Tena Mungu akasema, “Hii ndiyo alama ya agano ninalofanya kati yangu nanyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi kwa vizazi vyote vijavyo: 13naweka upinde wangu mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano kati yangu na dunia. 14Kila nitakapoifunika dunia kwa mawingu, na huo upinde wa mvua utakapoonekana katika mawingu, 15nitalikumbuka agano langu nanyi na viumbe vyote hai. Kamwe maji hayatageuka kuwa gharika ya kuviangamiza viumbe vyote hai. 16Huo upinde utakapotokea mawinguni, nitauona na kulikumbuka agano hilo la milele kati yangu na viumbe vyote hai duniani.” 17Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya agano ambalo nimefanya na viumbe vyote hai duniani.”#9:12-17 Agano hili lina alama ya kuonekana (kama vile tohara ilivyokuwa alama ya kuonekana kuhusu lile agano la Mungu na Abrahamu Mwa 17). Alama ina ubora wake kwa vile inakumbusha ahadi Mungu aliyofanya ya kutoleta tena gharika duniani.
Noa na wanawe
18Watoto wa Noa waliotoka katika safina walikuwa Shemu, Hamu na Yafethi.#9:18 Shemu, Hamu na Yafethi: Rejea Mwa 5:32; 6:10; 7:13; 10:1. Hamu ni baba wa Kanaani. Kuanzia karne ya 16 K.K. jina “Kanaani” lilitaja watu walioishi mijini na wafanyabiashara kwenye mwambao wa Palestina, kandokando ya bahari ya Mediteranea. Hamu alikuwa baba yake Kanaani. 19Hao ndio watoto watatu wa Noa, na kutokana nao watu walienea duniani kote.
20Noa alikuwa mkulima wa kwanza. Alilima shamba la mizabibu, 21akanywa divai, akalewa, kisha akalala uchi hemani mwake. 22Hamu, baba yake Kanaani, aliuona uchi wa baba yake, akatoka nje na kuwaambia ndugu zake wawili. 23Lakini Shemu na Yafethi wakatwaa nguo, wakaitanda mabegani mwao, wakaenda kinyumenyume na kuufunika uchi wa baba yao. Waliangalia pembeni, wala hawakuuona uchi wa baba yao. 24Noa alipolevuka na kujua alivyotendewa na mwanawe mdogo, 25akasema,
“Kanaani na alaaniwe!
Atakuwa mtumwa wa watumwa kwa ndugu zake.”
26Tena akasema,
“Shemu na abarikiwe na Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu!
Kanaani na awe mtumwa wake.
27Mungu na amkuze Yafethi,
aishi katika hema za Shemu;
Kanaani na awe mtumwa wake.”
28Baada ya gharika, Noa aliishi miaka 350, 29kisha akafariki akiwa na umri wa miaka 950.
Iliyochaguliwa sasa
Mwanzo 9: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993

: