Luka 22
22
Mpango wa kumwua Yesu
(Mat 26:1-5; Marko 14:1-2; Yoh 11:45-53)
1Sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia.#22:1 Kuhusu sikukuu ya Pasaka na ya mikate isiyotiwa chachu yafaa kukumbuka kwamba Pasaka ilidumu siku moja tu na ilifuatwa mara na sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu ambayo iliadhimishwa kwa siku saba. 2Makuhani wakuu na waalimu wa sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu, lakini waliwaogopa watu.
Yuda anakubali kumsaliti Yesu
(Mat 26:14-16; Marko 14:10-11)
3Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwaye Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili.#22:3 Yoh 13:2—4:27 Shetani: Ibilisi (Marko 1:13). Katika A.J. jina hilo lamaanisha mshtaki au mpinzani (wa Mungu). 4Yuda akaenda, akajadiliana na makuhani wakuu na walinzi wa hekalu kuhusu atakavyomsaliti Yesu kwao. 5Nao wakafurahi na kupatana naye kumlipa fedha. 6Yuda akakubali, na akawa anatafuta nafasi nzuri ya kumkabidhi kwao bila umati wa watu kujua.
Maandalio ya karamu ya Pasaka
(Mat 26:17-25; Marko 14:12-21; Yoh 13:21-30)
7Basi, siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa.#22:7 Kuadhimisha Pasaka watu walichinja kondoo ambaye walimla usiku wa kukumbuka kuondoka kwa Waisraeli nchini Misri (Kut 12:1-28). 8Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohane, akawaambia, “Nendeni mkatuandalie karamu ili tupate kula Pasaka.” 9Nao wakamwuliza, “Unataka tuiandae wapi?” 10Akawaambia, “Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia.#22:10-11 Kwa vile kawaida ni wanawake waliokuwa na desturi ya kubeba mtungi au kibuyu cha maji, kisa cha huyo mwanamume na mtungi wake wa maji kinaonesha kwamba Yesu alikwisha fanya mipango ya karamu ya mwisho. 11Mwambieni mwenye nyumba: ‘Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?’ 12Naye atawaonesheni chumba kikubwa ghorofani ambacho kimepambwa. Andalieni humo.” 13Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka.
Karamu ya Bwana
(Mat 26:26-30; Marko 14:22-26; 1 Kor 11:23-25)
14Saa#22:14 Saa: Yaani ya karamu ya Pasaka, ambayo ilianza kuadhimishwa mara ilipoanza siku ya 14 ya mwezi Nisani. (Taz 2:41 maelezo). ilipotimia, Yesu akakaa#22:14 Akakaa: Wakati huo watu hawakuwa wanatumia meza kama zetu ila walikaa wakiwa wameegemea vitu kama makochi. kula chakula pamoja na mitume wake. 15Akawaambia, “Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.”
17Kisha akatwaa kikombe cha divai, akashukuru, akasema, “Pokeeni, mgawane.#22:17 Luka peke yake ndiye anayetaja kikombe hapa kabla ya mkate (aya 19); lakini baadaye (aya 20) anataja kikombe kingine baada ya kula. Ama kweli, yaonekana kwamba katika karamu ya Pasaka watu walitumia kwa uchache hata vikombe vitatu vya divai. Wengine wanafikiri ni kwa sababu Luka alitaka kubainisha kati ya karamu ya Pasaka (aya 15-18) na ile ya “ukumbusho” ambayo Yesu aliadhimisha agano jipya na wafuasi wake (aya 19-20). 18Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.”
19Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka.”#22:19-20 Angalia pia sehemu nyingine sambamba katika Injili; linganisha Yoh 6:51-58. Baadhi ya hati za mkono za kale hazina sehemu ya aya 19 kuanzia na maneno: unaotolewa … na aya yote ya 20. Katika hati hizo ni kikombe kimoja tu kinatolewa na kufuatiliwa na mkate. 20Akafanya vivyo hivyo na kikombe cha divai baada ya chakula, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya#22:20 Agano Jipya: Yer 31:31-34 linalothibitishwa kwa damu yangu. Agano la kwanza (au mkataba) ambalo Mungu alifanya na Waisraeli lilithibitishwa kwa damu ya wanyama wa tambiko (Kut 24:6-8; Ebr 9:18-23). Ling Ebr 10:29; 13:20. Hili jipya linathibitishwa kwa kifo chake Yesu. linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.
21“Lakini, tazameni! Yule atakayenisaliti yuko nami hapa mezani.#22:21 Zab 41:9 Waandishi wengine wa Injili wanavyoeleza tukio la karamu ya Pasaka inakuwa kana kwamba Yuda hakuwako wakati Yesu alipozindua karamu hiyo; lakini Luka anatufanya tuelewe kwamba Yuda alikuwako. Maneno “atakayenisaliti” yanakumbusha Zab 41:9. 22Kweli Mwana wa Mtu anakwenda kuuawa kama ilivyopangwa,#22:22 Anakwenda kuuawa kama ilivyopangwa: Yaani Mungu ndiye aliyepanga hayo. lakini ole wake mtu anayemsaliti.”
23Hapo wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao atakayefanya jambo hilo.
Ubishi juu ya ukuu
24Kulitokea ubishi kati ya hao mitume kuhusu nani miongoni mwao anayefikiriwa kuwa mkuu kuliko wengine. 25Yesu akawaambia, “Wafalme wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, nao huitwa wafadhili#22:25 Wafadhili: Wagiriki waliita hivyo miungu yao, wafalme wao na watu wengine waliokuwa mashuhuri. wa watu. 26Lakini isiwe hivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenu ni lazima awe mdogo wa wote, na aliye kiongozi lazima awe kama mtumishi. 27Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.
28“Nyinyi ndio mliobaki nami wakati wote wa majaribu yangu; 29na, kama vile Baba yangu alivyonikabidhi ufalme, vivyo hivyo nami ninawakabidhi nyinyi ufalme. 30Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu na kuketi katika viti vya enzi kuyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
Yesu anabashiri kwamba Petro atamkana
(Mat 26:31-35; Marko 14:27-31; Yoh 13:36-38)
31“Simoni, Simoni! Sikiliza! Shetani alitaka kuwapepeta#22:31 Kuwapepeta: Msemo ambao unamaanisha kumtia mtu katika majaribio kuhusu uaminifu wake (Ling na Amo 9:9). nyinyi kama mtu anavyopepeta ngano. 32Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia,#22:32 Utakaponirudia: Msemo ambao waweza kueleweka kama kumgeukia Yesu au Mungu (yaani, kutubu baada ya kumkana Yesu). watie moyo ndugu zako.” 33Naye Petro akamjibu, “Bwana, mimi niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani, na hata kufa.” 34Yesu akamjibu, “Nakuambia wewe Petro, kabla jogoo hajawika leo utakuwa umenikana mara tatu.”#22:34 Kuhusu kuwika jogoo, yaonekana kwamba kadiri ya desturi (taratibu za Kiroma) yahusu kuwika jogoo mara ya kwanza usiku, yaani mwishoni mwa kesha la tatu ambalo liliishia yapata saa tisa usiku. Lakini hapa kuwika kwa jogoo ndiko kutakakokuwa ukumbusho kwa Petro (aya 74-75).
Wakati wa hatari
35Kisha, Yesu akawauliza wanafunzi wake, “Wakati nilipowatuma bila mfuko wa fedha wala mkoba wala viatu, mlitindikiwa chochote?” Wakajibu, “La.” 36Naye akawaambia, “Lakini sasa, yule aliye na mfuko wa fedha auchukue; na aliye na mkoba, hali kadhalika. Na yeyote asiye na upanga,#22:36 Mfuko wa fedha …mkoba … na upanga: Ni maneno yanayokumbusha hali ya safari ya hatari, alama ya majaribu ambayo yataanza kumpata Yesu na wanafunzi wake. auze koti lake anunue mmoja. 37Maana nawaambieni, haya maneno ya Maandiko Matakatifu: ‘Aliwekwa kundi moja na wahalifu,’ ni lazima yatimie. Naam, yale yanayonihusu yanafikia ukamilifu wake.” 38Nao wakasema, “Bwana, tazama; hapa kuna panga mbili.” Naye akasema, “Basi!”#22:38 Basi: Au: yatosha: Yaonekana kwamba wanafunzi hawakuelewa maana ya mfano wa maneno ya Yesu. Hivyo Yesu anakatiza mazungumzo yake nao.
Yesu anasali bustanini Gethsemane
(Mat 26:36-46; Marko 14:32-42)
39Yesu akatoka, na kama ilivyokuwa desturi yake, akaenda katika mlima wa Mizeituni; wanafunzi wake wakamfuata. 40Alipofika huko akawaambia, “Salini, msije mkaingia katika kishawishi.”#22:40 Kishawishi: (Hapa na katika aya 46). Majaribu yanayotajwa kuanzia aya 22:28-36 na jaribio gumu la aya 47. 41Kisha akawaacha, akaenda umbali wa mtu kuweza kutupa jiwe, akapiga magoti, akasali: 42“Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe#22:42 Kikombe: Kwa lugha ya mfano kumaanisha mateso au majaribio; taz maelezo katika Mat 26:39. hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu.” 43Hapo, malaika kutoka mbinguni akamtokea ili kumtia moyo.#22:43-44 Baadhi ya hati za mkono za kale maarufu hazina aya 43-44 ambazo hapa zimewekwa katika mabano mraba. Aya ya 44 inadhihirisha ukweli na nguvu ya mateso ya Yesu (taz Marko 14:33-34; Ebr 5:7-8). 44Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.
45Baada ya kusali, aliwarudia wanafunzi wake, akawakuta wamelala, kwani walikuwa na huzuni. 46Akawaambia, “Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika kishawishi.”
Yesu anatiwa nguvuni
(Mat 26:47-56; Marko 14:43-50; Yoh 18:3-11)
47Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu.#22:47-48 Kumbusu: Ilikuwa namna ya kusalimu kwa heshima kama vile ambavyo mwanafunzi alimfanyia mwalimu wake. 48Lakini Yesu akamwambia, “Yuda! Je, unamsaliti Mwana wa Mtu kwa kumbusu?” 49Wale wanafunzi wake walipoona hayo wakasema, “Bwana, tutumie panga zetu?” 50Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio lake la kulia.#22:50 Ling na Yoh 18:10,26. 51Hapo, Yesu akasema, “Acha! Hii inatosha.” Akaligusa sikio la mtu huyo, akaliponya.
52Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang'anyi? 53Nilipokuwa pamoja nanyi kila siku hekaluni hamkunitia nguvuni. Lakini, huu ndio wakati wenu hasa, ndio wakati wa utawala wa giza.”#22:53 Wakati wa utawala wa giza: Maneno yanayogusia ushindi wa muda wa nguvu za uovu; tazama pia Mate 26:18; lakini ushindi kamili wa mwisho ni wake Mungu (Yoh 1:5; Kol 1:13).
Petro anamkana Yesu
(Mat 26:57-58; Marko 14:53-54,66-72; Yoh 18:12-18,25-27)
54Basi, wakamkamata, wakamchukua na kwenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawa anamfuata nyuma kwa mbali. 55Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, nao wakawa wameketi pamoja, naye Petro akiwa miongoni mwao. 56Mtumishi mmoja wa kike alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, “Mtu huyu pia alikuwa pamoja na Yesu.” 57Lakini Petro akakana akisema, “Wee! Simjui mimi.” 58Baadaye kidogo, mtu mwingine akamwona Petro, akasema, “Wewe ni mmoja wao.” Lakini Petro akajibu “Bwana wee; si mimi!”
59Kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasisitiza, “Hakika huyu alikuwa pamoja naye; ametoka Galilaya ati.” 60Lakini Petro akasema, “Bwana wee; sijui hata unachosema!” Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.
61Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: “Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” 62Hapo akatoka nje, akalia sana.
Yesu anadhihakiwa na kupigwa
(Mat 26:67-68; Marko 14:65)
63Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki. 64Walimfunga kitambaa usoni, wakawa wanamwuliza, “Ni nani aliyekupiga? Hebu bashiri, tuone!” 65Wakamtolea maneno mengi ya matusi.
Yesu mbele ya Baraza
(Mat 26:59-66; Marko 14:55-64; Yoh 18:19-24)
66Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza#22:66 Baraza: Au: Halmashauri kuu ya Wayahudi. hilo. 67Nao wakamwambia, “Tuambie! Je, wewe ndiwe Kristo?” Lakini Yesu akawaambia, “Hata kama nikiwaambieni, hamtasadiki; 68na hata kama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu. 69Lakini tangu sasa, Mwana wa Mtu atakuwa ameketi upande wa kulia#22:69 Upande wa kulia: Zab 110:1; Mate 7:56. Ni mahali pa heshima. wa Mungu Mwenye Nguvu.”
70Hapo wote wakasema, “Ndiyo kusema wewe ni Mwana wa Mungu?” Naye akasema, “Nyinyi mnasema kwamba mimi ndiye.”#22:70 Jibu la Yesu laweza kueleweka ni kama mlivyosema au: nyinyi mmesema hivyo. 71Nao wakasema, “Je, tunahitaji ushahidi mwingine? Sisi wenyewe tumesikia akisema kwa mdomo wake mwenyewe.”
Iliyochaguliwa sasa
Luka 22: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993

: