Yohana 1
1
Yesu ni Neno la Mungu la Milele
1Mwanzoni Kabla ulimwengu haujaumbwa
alikuwepo Neno.#1:1 Neno Kwa Kiyunani neno hili ni logos, lenye maana mawasiliano ya aina yoyote. Linaweza kutafsiriwa “ujumbe”. Hapa lina maana ya Kristo; njia ambayo Mungu alitumia kuueleza ulimwengu kuhusu yeye. Pia katika mstari wa 10,14 na 16.
Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu,
na Neno alikuwa Mungu.
2Alikuwepo pamoja na Mungu
toka mwanzo.
3Kila kitu kilifanyika kupitia kwake.
Hakuna chochote katika uumbaji wa Mungu
kilichofanyika bila yeye.
4Ndani yake Neno kulikuwemo na uzima,
na uzima huo ulikuwa nuru
kwa ajili ya watu wa ulimwenguni.
5Nuru#1:5 Nuru Lenye maana ya Kristo, Neno, aliyeleta ulimwenguni uelewa kuhusu Mungu. Pia katika mstari wa 7. hiyo yamulika gizani,
na giza halikuishinda.#1:5 halikuishinda Au “kupotosha ukweli”.
6Alikuwepo mtu aliyeitwa Yohana, aliyetumwa na Mungu. 7Alikuja kuwaambia watu kuhusu nuru. Ili kupitia kwake watu wote waweze kusikia kuhusu yule aliye nuru na wamwamini. 8Yohana mwenyewe hakuwa nuru. Lakini alikuja kuwaambia watu kuhusu nuru.
9Nuru ya kweli,
anayeleta mwangaza kwa watu wote,
alikuwa tayari kuonekana kwa ulimwengu.
10Huyo Neno alikuwapo tayari ulimwenguni.
Ulimwengu uliumbwa kupitia yeye,
lakini ulimwengu haukumkubali.
11Alikuja kwa ulimwengu ulio wake,
na watu wake mwenyewe hawakumkubali.
12Lakini baadhi ya watu walimkubali wakamwamini
na akawapa haki ya kuwa watoto wa Mungu.
13Ndiyo, walikuwa watoto wa Mungu,
lakini si kwa kuzaliwa kimwili.
Haikuhusisha matamanio
ya kibinadamu.
Mungu mwenyewe aliwafanya
kuwa watoto wake.
14Neno akafanyika kuwa mwanadamu
na akaishi pamoja nasi.
Tuliouna ukuu wa uungu wake;
utukufu alionao Mwana pekee wa Baba.
15Yohana alizungumza kuhusu yeye alipopaza sauti na kusema, “Huyu ndiye niliyemzungumzia habari zake niliposema, ‘Anayekuja baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa sababu alikuwepo mwanzoni, zamani kabla sijazaliwa.’”
16Alikuwa amejaa neema na kweli ya Mungu,
tulipokea kutoka baraka moja
baada ya nyingine#1:16 baraka moja baada ya nyingine Kwa maana ya kawaida, “neema juu ya neema”. kutoka kwake.
17Hiyo ni kusema kuwa,
sheria ililetwa kwetu kupitia Musa.
Lakini neema na kweli imekuja
kupitia Yesu Kristo.
18Hakuna aliyewahi kumwona Mungu
isipokuwa Mwana peke yake,
ambaye yeye mwenyewe ni Mungu,
ametuonesha jinsi Mungu alivyo.
Yuko karibu sana na Baba
kiasi kwamba tunapomwona,
tumemwona Mungu.
Yohana Azungumza Juu ya Kristo
(Mt 3:1-12; Mk 1:1-8; Lk 3:1-9,15-17)
19Viongozi wa Kiyahudi kule Yerusalemu walituma baadhi ya makuhani na Walawi kwa Yohana kumwuliza, “Wewe ni nani?” Yohana akawaeleza kweli. 20Akajibu kwa wazi bila kusitasita, “Mimi siyo Masihi.”
21Wakamwuliza, “Sasa wewe ni nani? Je! wewe ni Eliya?”
Yohana akawajibu, “Hapana, mimi siye Eliya.”
Wakamwuliza tena, “Je! wewe ni Nabii?”#1:21 Nabii Huenda walikuwa na maana nabii ambaye Mungu, alimwambia Musa ya kwamba atamtuma. Tazama Kum 18:15-19. Pia katika mstari wa 25.
Naye akawajibu, “Hapana, mimi siyo nabii.”
22Kisha wakamwuliza, “Wewe ni nani basi? Tueleze habari zako. Tupe jibu la kuwaambia wale waliotutuma. Unajitambulisha mwenyewe kuwa nani?”
23Yohana akawaambia maneno ya nabii Isaya:
“‘Mimi ni mtu anayeipaza sauti yake toka nyikani:
Nyoosheni njia kwa ajili ya Bwana.’”#Isa 40:3
24Wale Wayahudi walitoka kwa Mafarisayo. 25Wakamwambia Yohana, “Unasema kuwa wewe siyo Masihi. Na unasema kuwa wewe siyo Eliya wala nabii. Sasa kwa nini unawabatiza watu?”
26Yohana akajibu, “Nawabatiza watu kwa maji. Lakini yupo mtu hapa kati yenu ambaye ninyi hamumjui. 27Yeye ndiye yule anayekuja baada yangu. Nami sina sifa za kuwa mtumwa anayefungua kamba za viatu vyake.”
28Mambo haya yote yalitokea Bethania iliyokuwa upande mwingine wa Mto Yordani. Hapa ndipo Yohana alipowabatiza watu.
Yesu, Mwanakondoo wa Mungu
29Siku iliyofuata Yohana akamwona Yesu akija kwake na kusema, “Tazama, Mwanakondoo wa Mungu mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu.” 30Huyu ndiye niliyezungumza habari zake niliposema, “Kuna mtu anayekuja baada yangu aliye mkuu zaidi yangu, kwa sababu yeye aliishi muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwangu.” 31Nami sikumjua yeye ni nani. Lakini nilikuja kuwabatiza watu kwa maji ili watu wa Israeli waelewe kuwa huyo ndiye Masihi.
32-34Kisha Yohana akasema maneno yafuatayo ili kila mtu asikie, “Mimi pia sikujua nani hasa alikuwa Masihi. Lakini yule aliyenituma kubatiza aliniambia, ‘Utamwona Roho akishuka na kutua kwa mtu. Huyo ndiye atakayewabatiza watu kwa Roho Mtakatifu.’ Nami nimeyaona haya yakitokea. Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama njiwa na kutulia juu ya mtu huyu. Hivyo haya ndiyo ninayowaambia watu: ‘Yeye huyo ndiye Mwana wa Mungu.’”#1:32-34 Yeye huyo ndiye Mwana wa Mungu Nakala zingine za kale kabisa za Kiyunani zina “Yeye ni mteule wa Mungu.”
Wafuasi wa Kwanza wa Yesu
35Siku iliyofuata Yohana alirejea tena mahali hapo pamoja na wafuasi wake wawili. 36Naye akamwona Yesu akitembea, hivyo akasema, “Angalieni, Mwanakondoo wa Mungu!”
37Wale wafuasi wake wawili walimsikia Yohana akisema haya, basi wakaondoka na kumfuata Yesu. 38Yesu aligeuka na kuwaona watu wawili wakimfuata. Akawauliza, “Mnataka nini?” Nao wakajibu wakimwuliza, “Rabi, unakaa wapi?” (Rabi tafsiri yake ni Mwalimu.)
39Yesu akajibu, “Njooni tufuatane pamoja nanyi mtapaona ninapokaa.” Hivyo wale watu wawili wakaenda pamoja naye. Wakaona mahali alipokuwa anakaa, nao wakashinda huko pamoja naye mchana wote. Hiyo ilikuwa ni saa kumi ya jioni.
40Watu hawa wakamfuata Yesu baada ya kusikia habari zake kutoka kwa Yohana. Mmoja wao alikuwa Andrea, nduguye Simoni Petro.
41Kitu cha kwanza alichokifanya Andrea kilikuwa ni kwenda kumtafuta ndugu yake Simoni. Andrea alipompata nduguye akamwambia, “Tumemwona Masihi.” (Masihi tafsiri yake ni Kristo.) 42Kisha Andrea akamleta Simoni nduguye kwa Yesu. Yesu akamtazama, na kumwambia, “Wewe ndiwe Simoni, mwana wa Yohana. Basi utaitwa Kefa.” (“Kefa” tafsiri yake ni “Petro”.#1:42 Petro Jina la Kiyunani “Petro”, kama jina la Kiaramu “Kefa”, linamaananisha “mwamba”.)
43Kesho yake Yesu akaamua kwenda Galilaya. Huko alikutana na Filipo na kumwambia, “Nifuate.” 44Filipo alikuwa mwenyeji wa mji wa Bethsaida, kama alivyokuwa Andrea na Petro. 45Filipo akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona mtu ambaye habari zake ziliandikwa na Musa katika sheria. Pia Manabii waliandika habari juu ya mtu huyu. Yeye ni Yesu, mwana wa Yusufu. Naye anatoka mjini Nazareti!”
46Lakini Nathanaeli akamwambia Filipo, “Nazareti! Je! inawezakana kupata kitu chochote chema kutoka Nazareti?”
Filipo akajibu, “Njoo uone.”
47Yesu akamwona Nathanaeli akija kwake na papo hapo akasema, “Mtu huyu anayekuja ni Mwisraeli halisi, ambaye unayeweza kumwamini.”#1:47 unayeweza kumwamini Kwa maana ya kawaida, “Ambaye ndani yake hamna hila.” Katika Agano la Kale, jina lingine la Israeli, Yakobo, linafafanuliwa kwa kutumia maneno kama vile “udanganyifu” au “hila”. Ambayo kwayo alijulikana sana. Tazama Mwa 27:35,36.
48Nathanaeli akamwuliza Yesu, “Umenifahamu kwa namna gani?”
Yesu akamjibu, “Nilikuona pale ulipokuwa chini ya mtini,#1:48 mtini Ama “mti wa mtini” aina ya mti wa matunda unaoitwa mtini. kabla Filipo hajakueleza habari zangu.”
49Kisha Nathanaeli akasema, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu. Nawe ni mfalme wa Israeli.” 50Yesu akamwambia, “Je! umeyaamini haya kwa sababu nimekwambia kuwa nilikuona chini ya mtini? Utaona mambo makubwa zaidi ya haya.” 51Kisha akasema, “Mniamini ninapowaambia kwamba mtaziona mbingu zimefunguka. Na mtawaona, ‘Malaika wa Mungu wakipanda juu na kushuka chini’#1:51 Mwa 28:12, ambayo ni sehemu ya simulizi kuhusu ndoto ya Yakobo ya ngazi iliyokuwa na malaika waliokuwa wakipanda na kushuka kati ya mbinguni na duniani. Tazama Mwa 28:10-17. kwa ajili Mwana wa Adamu.”
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 1: TKU
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Toleo la Awali
© 2017 Bible League International

: