Luka 3
3
Yohana Atayarisha Njia kwa Ajili ya Yesu
(Mt 3:1-12; Mk 1:1-8; Yh 1:19-28)
1Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, ambapo:
Pontio Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi;
Herode alikuwa mtawala wa Galilaya;
Filipo ndugu yake Herode alikuwa mtawala wa Iturea na Trakoniti;
na Lisania, alikuwa mtawala wa Abilene.
2Anasi na Kayafa walikuwa makuhani wakuu. Katika kipindi hiki, Yohana, mwana wa Zakaria, alikuwa akiishi jangwani na alipata ujumbe kutoka kwa Mungu. 3Alipita katika maeneo yote yaliyo karibu na Mto Yordani akiwahubiri watu ujumbe kutoka kwa Mungu. Aliwaambia wabatizwe kuonesha kuwa wamekubali kubadili maisha yao ndipo dhambi zao zitasamehewa. 4Hii ni kama maneno yaliyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya, yanayosema,
“Kuna mtu anayeipaza sauti yake kutokea nyikani:
‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana;
nyoosheni njia kwa ajili yake.
5Kila bonde litajazwa,
na kila mlima na kilima vitasawazishwa.
Barabara zilizopinda zitanyooshwa,
na barabara zenye mashimo zitasawazishwa.
6Na kila mtu ataona
jinsi Mungu atakavyowaokoa watu wake.’”#Isa 40:3-5
7Makundi ya watu walimwendea Yohana ili awabatize. Lakini aliwaambia, “Enyi nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia hukumu ya Mungu inayokuja? 8Badilisheni mioyo yenu! Kisha onesheni ya kuwa mmebadilika kwa namna mnavyoishi. Ninajua mtasema kuwa, ‘Abrahamu ni baba yetu.’ Hilo halijalishi chochote. Ninawaambia Mungu anaweza kumwumbia Abrahamu watoto kutokana na mawe haya! 9Na sasa shoka liko tayari kukata miti,#3:9 miti Watu wasiomtii Mungu ni kama miti itakayokatwa. kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni.”
10Watu wakamwuliza Yohana, “Tufanye nini?”
11Akajibu, “Ukiwa na mashati mawili mpe moja asiyekuwa na shati. Kama una chakula, kigawe pia.”
12Hata watoza ushuru walikuja kwa Yohana. Walitaka wabatizwe. Walimwambia, “Mwalimu, tufanye nini sisi?”
13Akawaambia, “Msitoze ushuru zaidi kuliko kiwango kilichoamriwa.”
14Askari wakamwuliza, “Vipi kuhusu sisi? Tufanye nini?”
Akawaambia, “Msitumie nguvu au kutengeneza mashtaka ya uongo ili watu wawape pesa. Mtosheke na mishahara mnayopata.”
15Kila mtu alitarajia kuja kwa Masihi,#3:15 Masihi Ni neno la Kiebrania lililo na maana sawa na Kristo kwa Lugha ya Kiyunani (Kigiriki), maana yake ni Mpakwa Mafuta. na walijiuliza wakisema, “Labda Yohana ndiye Masihi.”
16Yohana aliwajibu watu wote, akasema, “Ninawabatiza ninyi katika maji, lakini yupo mwingine anayekuja baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 17Yuko tayari sasa kuja kusafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri na makapi, na kuiweka katika ghala yake kisha ataichoma ile isiyofaa katika moto usiozimika.” 18Hivi ndivyo ambavyo Yohana aliwahubiri watu Habari Njema. Aliwaonya sana kuwa wanatakiwa kubadili njia zao.
Kazi ya Yohana Ilivyomalizika Baadaye
19Yohana alimkosoa Herode kwa sababu ya mambo mabaya aliyokuwa ameyafanya na Herodia, mkewe kaka yake Herode, na pia kwa mambo mengine mabaya aliyokuwa ameyafanya. 20Hivyo Herode aliongeza jambo jingine baya katika matendo yake maovu. Alimfunga Yohana gerezani.
Yohana Ambatiza Yesu
(Mt 3:13-17; Mk 1:9-11)
21Watu wote walipokuwa wakibatizwa, Yesu alikuja naye akabatizwa. Na alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka, 22na Roho Mtakatifu aliyekuwa katika umbo la njiwa akashuka juu yake. Sauti ikasikika toka mbinguni, “Wewe ni mwanangu, ninayekupenda, napendezwa nawe sana.”
Ukoo wa Yesu
(Mt 1:1-17)
23Yesu alipoanza kufundisha, alikuwa na umri kama wa miaka thelathini. Watu walidhani kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Yusufu.
Yusufu alikuwa mwana wa Eli.
24Eli alikuwa mwana wa Mathati.
Mathati alikuwa mwana wa Lawi.
Lawi alikuwa mwana wa Melki.
Melki alikuwa mwana wa Yana.
Yana alikuwa mwana wa Yusufu.
25Yusufu alikuwa mwana wa Matathia.
Matathia alikuwa mwana wa Amosi.
Amosi alikuwa mwana wa Nahumu.
Nahumu alikuwa mwana wa Esli.
Esli alikuwa mwana wa Nagai.
26Nagai alikuwa mwana wa Maathi.
Maathi alikuwa mwana wa Matathia.
Matathia alikuwa mwana wa Semei.
Semei alikuwa mwana wa Yusufu.
Yusufu alikuwa mwana wa Yoda.
27Yoda alikuwa mwana wa Yoana.
Yoana alikuwa mwana wa Resa.
Resa alikuwa mwana wa Zerubabeli.
Zerubabeli alikuwa mwana wa Shealtieli.
Shealtieli alikuwa mwana wa Neri.
28Neri alikuwa mwana wa Melki.
Melki alikuwa mwana wa Adi.
Adi alikuwa mwana wa Kosamu.
Kosamu alikuwa mwana wa Elmadamu,
Elmadamu alikuwa mwana wa Eri.
29Eri alikuwa mwana wa Yoshua.
Yoshua alikuwa mwana wa Eliezeri.
Eliezeri alikuwa mwana wa Yorimu.
Yorimu alikuwa mwana wa Mathati.
Mathati alikuwa mwana wa Lawi.
30Lawi alikuwa mwana wa Simeoni.
Simeoni alikuwa mwana wa Yuda.
Yuda alikuwa mwana wa Yusufu.
Yusufu alikuwa mwana wa Yonamu.
Yonamu alikuwa mwana wa Eliakimu.
31Eliakimu alikuwa mwana wa Melea.
Melea alikuwa mwana wa Mena.
Mena alikuwa mwana wa Matatha.
Matatha alikuwa mwana wa Nathani.
Nathani alikuwa mwana wa Daudi.
32Daudi alikuwa mwana wa Yese.
Yese alikuwa mwana wa Obedi.
Obedi alikuwa mwana wa Boazi.
Boazi alikuwa mwana wa Salmoni.#3:32 Salmoni Au “Sala”, kama ilivyo katika nakala za zamani za tafsiri ya Kiyunani ya Kale. Tazama Mt 1:4-5 na 1 Nya 2:11.
Salmoni alikuwa mwana wa Nashoni.
33Nashoni alikuwa mwana wa Aminadabu.
Aminadabu alikuwa mwana wa Admini,
Admini alikuwa mwana wa Aramu.#3:33 Aramu Baadhi ya nakala za Kiyunani zina “Arni” au “Ramu”; majina mengine ya Aramu.
Aramu alikuwa mwana wa Hesroni.
Hesroni alikuwa mwana wa Peresi.
Peresi alikuwa mwana wa Yuda.
34Yuda alikuwa mwana wa Yakobo.
Yakobo alikuwa mwana wa Isaka.
Isaka alikuwa mwana wa Abrahamu.
Abrahamu alikuwa mwana wa Tera.
Tera alikuwa mwana wa Nahori.
35Nahori alikuwa mwana wa Serugi,
Serugi alikuwa mwana wa Ragau.
Ragau alikuwa mwana wa Pelegi.
Pelegi alikuwa mwana wa Eberi,
Eberi alikuwa mwana wa Sala.
36Sala alikuwa mwana wa Kenani.
Kenani alikuwa mwana wa Arfaksadi.
Arfaksadi alikuwa mwana wa Shemu.
Shemu alikuwa mwana wa Nuhu.
Nuhu alikuwa mwana wa Lameki.
37Lameki alikuwa mwana wa Methusela.
Methusela alikuwa mwana wa Henoko.
Henoko alikuwa mwana wa Yaredi.
Yaredi alikuwa mwana wa Mahalaleli.
Mahalaleli alikuwa mwana wa Kenani.
38Kenani alikuwa mwana wa Enoshi.
Enoshi alikuwa mwana wa Sethi.
Sethi alikuwa mwana wa Adamu.
Adamu alikuwa mwana wa Mungu.
Iliyochaguliwa sasa
Luka 3: TKU
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Toleo la Awali
© 2017 Bible League International

:
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Toleo la Awali
© 2017 Bible League International