Mathayo 15:25-27
Mathayo 15:25-27 TKU
Ndipo mwanamke alikuja mahali alipokuwa Yesu na kuinama mbele yake. Akasema, “Bwana, nisaidie!” Akamjibu kwa kumwambia, “Si sahihi kuwapa mbwa mkate wa watoto.” Mwanamke akasema, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula vipande vya chakula vinavyoanguka kutoka kwenye meza za mabwana zao.”