Mwanzo 25
25
Wazawa wa Ketura
1Abrahamu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura. 2#1 Nya 1:32 Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua.
3Yokshani akamzaa Sheba, na Dedani; na wana wa Dedani walikuwa Waashuri na Waletushi, na Waleumi.
4Na wana wa Midiani walikuwa, Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa.
Hao wote walikuwa ni wana wa Ketura.
5 #
Mwa 24:36
Abrahamu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo. 6#Mwa 21:14; Amu 6:3 Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Abrahamu, Abrahamu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
Kifo cha Abrahamu
7Abrahamu aliishi miaka mia moja na sabini na mitano. 8#Mwa 15:15; 47:8,9; 35:29; 49:33; Mdo 13:36 Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake. 9#Mwa 49:29,30; 50:13 Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, lielekealo Mamre. 10#Mwa 23:3-16 Katika lile shamba alilolinunua Abrahamu kwa wazawa wa Hethi, huko ndiko alikozikwa Abrahamu na Sara mkewe.
11 #
Mwa 16:14; 24:62 Ikawa, baada ya kufa kwake Abrahamu, Mungu akambariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akakaa karibu ya Beer-lahai-roi.
Uzao wa Ishmaeli
12 #
1 Nya 1:29
Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli, mwana wa Abrahamu, ambaye Hajiri, Mmisri, mjakazi wa Sara, alimzalia Abrahamu. 13Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao.
Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu, 14na Mishma, na Duma, na Masa, 15na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema. 16#Mwa 17:20 Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.
17 #
Mwa 25:8; 49:33; Mk 15:37 Ishmaeli aliishi miaka mia moja na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.
18 #
1 Sam 15:7; Mwa 16:12 Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote.
Kuzaliwa na kukua kwa Esau na Yakobo
19 #
Mt 1:2
Na hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Abrahamu. Abrahamu alimzaa Isaka. 20#Mwa 22:23; 24:29,67 Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.
21 #
1 Sam 1:11; 1 Nya 5:20; 2 Nya 33:13; Ezr 8:23; Rum 9:10 Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba. 22#1 Sam 9:9; 10:22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. 23#Rum 9:12; Mwa 24:60 BWANA akamwambia,
Mataifa mawili yako tumboni mwako,
Na makabila mawili ya watu watafarakana tangu tumboni mwako.
Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,
Na mkubwa atamtumikia mdogo.
24Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake. 25#Mwa 27:11 Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. 26#Hos 12:3; Mwa 27:36 Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa. 27#Mwa 27:3,5; Ayu 1:1,8; 2:3; Ebr 11:9 Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani. 28#Mwa 27:6,19 Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo.
Esau auza haki ya uzaliwa wake
29Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka mbugani, naye alikuwa amechoka sana. 30Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.#25:30 Edomu: maana yake ni Mwekundu. 31Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza. 32Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? 33#Ebr 12:16 Yakobo akamwambia, Niapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. 34#1 Kor 15:32 Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
Iliyochaguliwa sasa
Mwanzo 25: RSUVDC
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.

: