Mwanzo 7
7
Gharika kuu
1 #
Zab 91:1-10; Ebr 11:7; 1 Pet 3:20; 2 Pet 2:5,9; Mwa 6:9; Zab 33:18,19 BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. 2#Law 11:1-31 Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, wa kiume na wa kike; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, wa kiume na wa kike. 3Tena katika ndege wa angani saba saba, wa kike na wa kiume; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote. 4#Ayu 22:16; 2 Pet 2:5 Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali. 5#Mwa 6:22; Zab 119:6 Nuhu akafanya kama vile BWANA alivyomwamuru.
6Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi. 7#Mt 24:38-39; Lk 17:27; Ebr 6:18 Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika. 8Na katika wanyama walio safi, na wanyama wasio safi, na ndege, navyo vyote vitambaavyo juu ya nchi, 9wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kike na wa kiume, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu. 10Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi. 11#2 Pet 3:6; Mwa 8:2; Mit 8:28; Eze 20:19; Zab 78:23; Isa 24:18; Mal 3:10 Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka. 12Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku. 13Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye; 14wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yoyote. 15Waliingia katika safina alimokuwa Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake. 16#Zab 91:1-16; 17:8; 145:20; 1 Pet 1:5 Na walioingia, waliingia wa kike na wa kiume, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia.
17Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini; nayo maji yakazidi, yakaifanya safina ielee, ikaelea juu ya nchi. 18#Zab 104:26 Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi; na safina ikaelea juu ya uso wa maji. 19#Zab 104:6 Maji yakazidi kuongezeka sana sana juu ya nchi; hata milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikwa. 20Maji yakaongezeka hata milima ikafunikwa kiasi cha dhiraa kumi na tano. 21#Mwa 6:13,17; Ayu 22:16; Mt 24:39; Lk 17:27; 2 Pet 3:6 Wakafa watu wote waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; 22#Mwa 2:7 kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. 23#Eze 14:14; Mal 3:17,18; Ebr 11:17; 1 Pet 3:20; 2 Pet 2:5 Kila kilichokuwa hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali; mwanadamu, wanyama wa kufugwa, kitambaacho na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao waliokuwa pamoja naye katika safina. 24#Mwa 8:3,4 Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.
Iliyochaguliwa sasa
Mwanzo 7: RSUVDC
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.

: