Yohana 9
9
Mtu aliyezaliwa kipofu apata kuona
1 #
Mdo 3:2; 14:8 Na alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. 2#Lk 13:2; Kut 20:5 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? 3#Yn 11:4 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. 4#Yn 5:17,20; 11:9 Imenipasa kuzifanya kazi zake Yeye aliyenituma maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. 5#Mt 5:14; Yn 8:12; 12:35 Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. 6#Mk 8:23 Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope machoni, 7akamwambia, Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi akiwa anaona. 8Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba? 9Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. 10Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje? 11Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona. 12Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.
Mafarisayo wauchunguza uponyaji
13Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani. 14#Yn 5:9 Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho. 15Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona. 16#Yn 3:2; 7:43; 9:31,33 Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa na utengano kati yao. 17#Yn 4:19 Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje kuhusu habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii. 18Basi Wayahudi hawakuamini habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hadi walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona. 19Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye mwana wenu, ambaye mnasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona sasa? 20Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu, tena ya kuwa alizaliwa kipofu; 21lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe. 22#Yn 7:13; 12:42; 16:2 Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kukubaliana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi. 23Ndiyo sababu wale wazazi wake walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.
24 #
Yos 7:19
Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi. 25Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nilikuwa kipofu na sasa naona. 26Basi wakamwambia, Alikutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani? 27Akawajibu, Nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake? 28Basi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake yule; sisi tu wanafunzi wa Musa. 29Sisi tunajua ya kuwa Mungu alisema na Musa; bali yule hatujui atokako. 30Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho! 31#Isa 1:15; Mit 15:29; Mdo 10:35 Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. 32Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya mtu, ambaye alizaliwa kipofu. 33#Yn 9:16 Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lolote. 34#Yn 9:2; Zab 51:5 Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.
Upofu wa kiroho
35Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? 36Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? 37#Yn 4:26; 10:25 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. 38Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia. 39#Mt 13:11-15 Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu. 40#Mt 15:14; 23:26 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu? 41#Mit 26:12 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini kwa kuwa sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 9: RSUVDC
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.

: