Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 1

1
1KITABU kile cha kwanza nalikifanya, Theofilo, katika khabari ya mambo yote aliyoanza kufanya Yesu na kufundisha, 2hatta siku ile alipowaagiza kwa Roho Mtakatifu mitume aliowachagua, akachukuliwa juu: 3na baada ya kuteswa kwake, akawadhihirisbia ya kwamba yu hayi, kwa dalili nyingi, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyonkhusu ufalme wa Mungu. 4Hatta, akikutana nao, akawaagiza wasitoke katika Yerusalemi, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia khabari zake kwangu; 5ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi. 6Bassi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Bwana, wakati huu ndipo unapomrudishia Israeli ufalme wake? 7Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. 8Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi. 9Akiisha kusema haya, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 10Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, 11wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
12Kiisha wakarudi kwenda Yerusalemi kutoka mlima ulioitwa wa mizeituni, ulio karibu na Yerusalemi, wapata mwendo wa sabato. 13Hatta walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartolomayo na Mattayo, Yakobo wa Alfayo, na Simon Zelote, na Yuda wa Yakobo. 14Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kuomba, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama wake Yesu, na ndugu zake.
15Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini), 16Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, 17akapata sehemu ya khuduma hii. 18(Bassi huyu alinunua konde kwa ijara ya ndhalimu; akaanguka kifudifudi akapasuka, matumbo yake yote yakatoka. 19Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemi; hatta konde lile likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.) 20Kwa maana imeandikwa katika kitabu cha Zaburi, Kikao chake kiwe ukiwa, wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine. 21Bassi katika watu waliofuatana nasi wakati wote ambapo Bwana Yesu alikuwa akiingia kwetu na kutoka kwetu, 22akianza tangu ubatizo wa Yohana, hatta siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, lazima mmoja wao afanywe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi. 23Wakaweka wawili, Yusuf, aitwae Barsaba, aliyepewa jina la pili Yusto, na Mattiya. 24Wakasali, wakasema, Wewe, Bwana, ujuae mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, 25atwae sehemu yake ya khuduma hii na utume huu, alioukosa Yuda aende zake mahali pake. 26Wakawapigia kura: kura ikamtoa Mattiya; akachaguliwa kuwa pamoja na mitume edashara.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo 1: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia