Matendo 16
16
1AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani. 2Mtu huyo alishuhudiwa na ndugu waliokaa Lustra na Derbe. 3Paolo akamtaka huyu afuatane nae, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile: kwa maana wote walijua ya kuwa baba yake ni Myunani. 4Bassi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemi, illi wazishike. 5Makanisa yakatiwa nguvu kwa imani, hesabu yao ikaongezeka killa siku.
6Wakapita katika inchi ya Frugia na Galatia, wakakatazwa na Roho Mtakatifu, wasilikhubiri Neno katika Asia. 7Walipofika kukabili Musia, wakajaribu kwenda Bithunia, lakini Roho ya Yesu hakuwapa rukhusa, 8wakapita Musia wakatelemkia Troa. 9Paolo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi akimwambia, Vuka uje Makedonia utusaidie. 10Bassi alipokwisha kuona yale maono, marra tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Bwana ametuita tuwakhubiri Injili.
11Tukangʼoa nanga kutoka Troa, tukafika Samothraki kwa tanga moja. 12Siku ya pili tukafika Neapoli na kutoka hapo tukafika Filippi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika wilaya ile, nayo ni Kolonia ya Kirumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. 13Hatta siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, tukidhani ya kuwa hapo pana mahali pii kuomba; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. 14Mwanamke mnioja, jina lake Ludia, mwenye kuuza rangi ya zambarao, mwenyeji wa Thuatira, mcha Mungu, akatusikiliza. Moyo wake huyu ukafunguliwa na Bwana, ayaangalie mineno yaliyonenwa na Paolo. 15Hatta alipokwisha kumbatiza, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae; akatushurutisha. 16Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kuombea, kijakazi kimoja aliyekuwa na pepo ya Puthoni akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kutabiri. 17Akamfuata Paolo na sisi, akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kutukhubiri njia ya wokofu. 18Akawa akifanya hayo siku nyingi. Lakini Paolo akakasirika akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. 19Bassi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paolo na Sila, wakawakokota hatta sokoni mbele ya wakuu wa mji; 20wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanataharakisha mji wetu, nao ni Wayahudi. 21Tena wanatangaza khabari ya desturi zisizo halali kwetu tuzipokee wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi. 22Makutano wote wakaondoka wakawaendea, Makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.
23Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. 24Nae akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. 25Lakini panapo usiku wa manane Paolo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza. 26Ghafula pakawa tetemeko kuu la inchi, hatta misingi ya gereza ikatikisika, na marra hiyo milango ikafunguka, vifungo vya watu wote vikalegezwa. 27Yule mlinzi wa gereza akaamka, akaona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, akafuta upanga wake, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. 28Paolo akapaaza sauti yake kwa uguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. 29Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa khofu, akawaangukia miguu Paolo na Sila; 30kiisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka? 31Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka pamoja na uyumba yako. 32Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. 33Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, akahatizwa, yeye ua watu wote wa nyumbani mwake wakati huohuo. 34Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.
35Kulipopambazuka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao. 36Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paolo maneno haya ya kama, Makadhi wametuma watu kuwafungulieni! bassi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani. 37Paolo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, teua wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? la, sivyo, na waje wenyewe wakatutoe. 38Wakubwa wa askari wakawapasha makadhi khabari za maneno haya: nao wakaogopa, waliposikia ya kwamba ni Warumi. 39Wakaja wakawasihi: na walipokwisha kuwatoa nje, wakawaomba watoke katika mji ule. 40Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Ludia; na walipokwisha kuwaona ndugu wakawafariji, wakaenda zao.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 16: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: