Matendo 4
4
1HATTA walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, 2wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuukhubiri ufufuo wa wafu unaopatikana kwa Yesu. 3Wakawakamata, wakawaweka garezani hatta assubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni. 4Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini: na hesabu ya watu ilikuwa kama elfu tano.
5Hatta assubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemi, 6na Kayafa pia, na Yohana, na Iskander, na wo wote waliokuwa jamaa zake kuhani mkuu. 7Wakawaweka katikati, wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani mmefanya haya ninyi? 8Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, 9Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, kama tukiulizwa leo khabari ya yule mtu dhaifu jinsi alivyoponywa, 10jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu. 11Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. 12Wala hakuna wokofu katika mwingine aliye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wana Adamu litupasalo kuokolewa nalo.
13Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.
14Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. 15Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri, wakisemii, Tuwafanyieni watu hawa? 16maana ishara mashuhuri imefanywa nao, iliyo dhabiri kwa watu wote wakaao Yerusalemi, wala hatuwezi kuikana. 17Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, tuwaogofishe wasiseme tena na mtu aliye yote kwa jina hili. 18Wakawaita, wakawaagiza wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. 19Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, 20Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. 21Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka: 22maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arubaini.
23Hatta walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha khabari ya mambo yote waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee. 24Nao waliposikia, wakampaazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na inchi na bahari na vitu vyote vilivyomo: 25nawe ulinena kwa kinywa cha Daud mtumishi wako,
Mbona mataifa wamefanya ghasia,
Na watu wametafakari ubatili?
26Wafalme wa dunia wamejipanga,
Na wakuu wamefanya shauri pamoja,
Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.
27Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, 28illi wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. 29Bassi sasa, Bwana, yaangalie maogofya yao; ukawajalie watumishi wako kunena neno lako kwa uthabiti, 30ukinyosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu zifanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu. 31Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.
32Na jamii ya watu walioamini walikuwa moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. 33Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa uguvu nyingi. Neema nyingi ikawa juu yao wote. 34Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na uwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa 35wakaiweka miguuni jia mitume; killa mtu akagawiwa kwa kadiri alivyohitaji. 36Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro, 37alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 4: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: