Matendo 6
6
1HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku. 2Wale thenashara wakawaita jamii va wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kukhudumu mezani. 3Bassi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, illi tuwaweke juu ya jambo hili: 4na sisi tutadumu katika kumwomba Mungu na kulikhudumia Neno lake. 5Neno hili likapendeza machoni jia mkutano wote: wakamehagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu na Filipo, na Prokoro, na Nikanor, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia. 6Wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.
7Nenu la Mungu likaenea: hesahu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemi: jamii kubwa la makuhani wakaitii Imani.
8Na Stefano, akijaa imani na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. 9Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano: 10lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala na Roho aliyosema nayo. 11Hatta wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. 12Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi: wakaniwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. 13Wakasimamisha mashahidi wa uwongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati: 14maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu pahali hapa, na kuzihadili desturi tulizopewa na Musa. 15Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 6: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: