Yohana MT. 12
12
1BASSI Yesu siku sita kabla ya Pasaka akafika Bethania, hapo alipokuwapo Lazaro, yule aliyekufa akaihfuliwa nae. 2Bassi wakamfanyizia karamu huko; Martha akakhudumu. Na Lazaro alikuwa mmoja wa wale walioketi chakulani pamoja nae. 3Bassi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akaifuta miguu yake kwa nywele zake; nyumha ikajaa harufu ya yale marhamu. 4Bassi Yuda Iskariote, mwana wa Simon, mmoja wa wanafunzi wake, aliye tayari kumsaliti, akanena, 5Mbona marhamu haya hayakuuzwa kwa dinari mia tatu, na kupewa maskini? 6Aliyasema haya, si kwa kuwahurumia maskini; hali kwa kuwa ni mwizi, nae ndiye aliyeshika mfuko, akavichikua vilivyotiwa humo. 7Bassi Yesu alisema, Mwache, ameyaweka haya kwa siku ya maziko yangu. 8Maana maskini mnao siku zote pamoja nauyi; bali mimi hamnami siku zote. 9Bassi kundi kubwa la Wayuhudi walijua ya kuwa yeye yuko huko; wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, bali wamwone na Lazaro, ambae alimfufua katika wafu. 10Makuhani wakuu wakafanya shauri wamwue Lazaro nae; 11maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walikwenda zao, wakamwamini Yesu.
12Siku ya pili watu wengi walioijia siku kuu, waliposikia kwamba Yesu anakuja Yerusalemi, 13wakatwaa matawi ya mitende wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana; Amebarikiwa ajiie kwa jina la Bwana, mfalme wa Israeli. 14Yesu akapata mwana punda, akampanda, kama ilivyoandikwa, 15Usiogope, binti Sayuni: angalia, Mfalme wako anakuja, ameketi juu ya mwana wa punda. 16Mambo haya wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walikumbuka ya kwamba ameandikiwa haya na ya kwamba walimtendea haya. 17Bassi wakamshuhudia makutano waliokuwa pamoja nae alipomwita Lazaro kutoka kaburini akamfufua. 18Kwa sababu hiyo makutano wakaenda kumlaki, kwa sababu wamesikia ya kwamba amefanya ishara hii. 19Bassi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno: tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.
20Na palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliopanda kwenda kuabudu wakati wa siku kuu. 21Bassi hao walimwendea Filipo wa Bethsaida wa Galilaya, wakimwuliza, wakisema, Bwana, tunataka kumwona Yesu. 22Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kiisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. 23Yesu akajibu, akinena, Saa imefika, atukuzwe Mwana wa Adamu. 24Amin, amin, nawaambieni, Punje ya nganu isipoanguka katika inchi ikafa, hukaa katika hali ya peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi. 25Aipendae roho yake ataiangamiza; nae aichukiae roho yake katika ulimwengu huu ataihifadhi hatta uzima wa milele. 26Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu. 27Sasa roho yangu imefadhaika; niseme nini? Baba, uniokoe na saa hii. Lakini kwa ajili ya hayo naliifikia saa hii. Baba, ulitukuze jina lako. 28Bassi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. 29Bassi makutano waliosimama karibu wakasikia, wakanena kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema nae. 30Yesu akajibu, akasema, Sauti hii haikuwa kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu. 31Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa mkuu wa ulimwengu him atatupwa nje. 32Nami nikiinuliwa juu ya inchi nitavuta wote kwangu. 33Alinena haya, illi kuonyesha ni mauti gani atakayokufa. 34Bassi makutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hatta milele: nawe wanenaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani? 35Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako. 36Maadam mnayo nuru, iaminini nuru, mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake akajificha nao.
37Lakini ijapokuwa amefanya ishara kubwa namna hii mbele yao, hawakumwamini; 38illi litimizwe lile neno la nabii Isaya alilolisema,
Bwana, nani aliyeziamini khabari zetu?
Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? 39Kwa sababu hii hawakuweza kuamini, kwa sababu Isaya alisema tena,
40Amewapofusba macho, amefanya migumu mioyo yao,
Wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao,
Wakagenka, nikawaponya.
41Maneno hayo aliyasema Isaya alipouona utukufu wake, akataja khabari zake. 42Walakini hatta katika wakubwa wengi walimwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumwungama, wasije wakalolewa katika masunagogi. 43Kwa maana waliupenda utukufu wa wana Adamu kuliko utukufu wa Mungu.
44Yesu akapaaza sauti yake akasema, Aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka. 45Nae anitazamae mimi, amtazama yeye aliyenipeleka. 46Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani. 47Na mtu akisikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu. 48Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 49Kwa maana mimi sikusema kwa nafsi yangu tu; bali yeye aliyenipeleka, yaani Baba, ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. 50Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele: bassi haya ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana MT. 12: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: