Yohana MT. 16
16
1MANENO haya nimewaambieni msije mkachukizwa. 2Watawaharamisha masunagogi: naam, saa inakuja, atakapodhani killa mtu awauae kuwa amtolea Mungu ibada. 3Na hayo watawatendeni kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. 4Lakini nimewaambieni haya, illi kusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambieni. Haya sikuwaambieni tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwa pamoja nanyi.
5Lakini sasa nakwenda zangu kwake aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizae, Unakwenda zako wapi? 6Illa kwa sababa nimewaambieni haya, huzimi imejaa mioyoni mwenu. 7Lakini mimi nawaambieni iliyo kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke: kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 8Na akiisha kuja yeye, atauhakikisha ulimwengu kwa khabari ya dhambi, na haki, na hukumu; 9Kiva khabari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 10kwa khabari ya haki, kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11kwa khabari ya hukumu, kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amehukumiwa. 12Hatta ninayo mengi bado ya kuwaambieni, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. 13Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake. 14Yeye atanitukuza mimi: kwa kuwa atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari. 15Yote aliyo nayo Baba m yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari.
16Bado kitambo, nanyi hamnioni tena; na bado tena kitambo, na mtaniona. Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba. 17Bassi baadhi ya wanafunzi wake walisemezana, Neno gani hili analosema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo na mtaniona? na, Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba? 18Bassi walisema. Neno gani hili analosema, hili Bado kitambo? Hatujui asemalo. 19Yesu alifahamu ya kwamba walitaka kumwuliza akawaambia, Hili ndilo mnalotafuta ninyi kwa ninyi, ya kuwa nalisema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na bado kitambo na mtaniona? 20Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mtalia, na kuomboleza, bali, ulimwengu utafurahi: ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha, 21Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imekuja; hatta, akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena shidda, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. 22Bassi na ninyi sasa hivi mna huzuni; lakini nitawaona tena, na moyo wenu utafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleae.
23Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni. 24Mpaka leo hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, na mtapata, furaha yenu iwe timilifu. 25Haya nimesema nanyi kwa methali: saa inakuja, sitasema nanyi tena kwa methali, lakini nitawapa kwa wazi khabari ya Baba. 26Katika siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea Baba; 27kwa maana Baba mwenyewe awapenda ninyi, kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, mkaamini ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. 28Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba. 29Wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni methali yo yote. 30Sasa tumejua ya kuwa unajua yote, wala huhitaji mtu akuulize; kwa hiyo twaamini ya kwamba ulitoka kwa Mungu. 31Yesu akawajihu, Sasa hivi mnaamini? 32Saa inakuja, naam, imekwisha kuja, mtatawanyika killa mmoja kwa mambo yake, mtaniacha mimi peke yangu; wala mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. 33Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana MT. 16: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: