Yohana MT. 6
6
1BAADA ya haya Yesu alikwenda zake ngʼambu ya bahari ya Galilaya, bahari ya Tiberia. 2Makutano mengi wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. 3Yesu akapanda mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. 4Na Pasaka, siku kuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu. 5Bassi Yesu alipoinua macho yake akaona makutano mengi yanakuja kwake, akamwambia Filipo, Tununue wapi mikate, hawa wapate kula? 6Alinena haya illi amjaribu: kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. 7Filipo akamjibu, Mikate ya dinari miateen haiwatoshi, killa mmoja apate kidogo tu. 8Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu wa Simon Petro, akamwambia, 9Yupo mtoto hapa, ana mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini haya nini kwa watu wengi kama hivi? 10Yesu akasema, Waketisheni watu. Palikuwako majani tele mahali pale. Bassi watu waume wakaketi, jumla yao wapata elfu tano. 11Bassi Yesu akaitwaa mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. 12Waliposhiba, akawaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kitu kisipotee. 13Bassi wakavikusanya, wakajaza vikapu thenashara kwa vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia waliokula. 14Bassi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya Yesu, wakasema, Huyu hakika ni nabii yule ajae ulimwenguni.
15Bassi Yesu, akitambua ya kuwa walitaka kuja kumchukua illi wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani, yeye peke yake.
16Hatta ilipokuwa jioni, wanafunzi wake wakatelemka baharini: 17wakapanda chomboni wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaum. Na giza imekwisha kuwa, nae Yesu hajawafikia. 18Bahari ikaanza kuchafuka, upepo mwingi ukivuma. 19Bassi wakavuta makasia kadiri ya stadio ishirini na tano au thelathini, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari, anakikaribia chombo: wakaogopa. 20Nae akawaambia. Ni mimi, msiogope. 21Bassi wakataka kumpokea chomboni; na marra hiyo chombo kikaifikilia inchi waliyokuwa wakienda.
22Siku ya pili yake makutano waliosimama ngʼambu ya bahari wakaona ya kuwa hakuna mashua nyingine huko illa ile moja waliyoingia wanafunzi wake; tena ya kuwa Yesu hakuingia katika mashua ile pamoja na wanafunzi wake, bali wanafunzi wake walikwenda peke yao, 23(lakini mashua nyingine zilikuja kutoka Tiberia karibu na pahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aiiposhukuru); 24bassi makutano walipoona ya kuwa Yesu hakuwako huko wala wanafunzi wake, wenyewe wakaingla vyomboni, wakaenda Kapernaum wakimtafuta Yesu. 25Hatta walipomwona ngʼambu ya bahari, wakamwambia, Rabbi, umekuja lini hapa? 26Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate, mkashiba. 27Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu. 28Bassi wakamwambia, Tufanyeje tupate kuzitenda kazi za Mungu? 29Yesu akajibu, akawaambia, Hii ni kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa nae. 30Wakamwambia, Unafanya ishara gani bassi illi tuone tukaamini? Unatenda kazi gani? 31Baba zetu waliila manna jangwani, kama ilivyoandikwa, Aliwapa mkate kutoka mbinguni wale. 32Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa mkate ule kutoka mbinguni, bali Baba yangu anawapa mkate ule utokao mbinguni ulio wa kweli. 33Kwa maana mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. 34Bassi, wakamwambia, Bwana, siku zote utupe mkate huo. 35Yesu akawaambia, Mimi ni mkate wa uzima; yeye ajae kwangu hataona njaa kabisa, nae aniaminiye hataona kiu kamwe. 36Lakini naliwaambieni ya kwamba mmeniona bila kuniamini. 37Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe. 38Kwa kuwa sikushuka kutoka mbinguni illi niyafanye mapenzi yangu, hali mapenzi yake aliyenipeleka. 39Na mapenzi yake Baba aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika vyote alivyonipa nisipoteze kitu hatta kimoja, hali nikifufue siku ya mwisho. 40Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.
41Bassi Wayahudi wakamnungʼunikia, kwa sababu alisema, Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni. 42Wakanena, Huyu siye Yesu, mwana wa Yusuf, ambae twamjua baba yake na mama yake? Bassi, anenaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni? 43Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Msinungʼunike ninyi kwa ninyi. 44Hakuna mtu awezae kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka: nami nitamfufua siku ya mwisho. 45Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Bassi killa aliyesikia na kujifunza kwa Baba, huja kwangu. 46Si kwamba mtu amemwona Baba, illa yeye atokae kwa Mungu huyu ndiye aliyemwona Baba. 47Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi ana uzima wa milele. 48Mimi ni mkate wa uzima. 49Baba zetu waliila manna jangwani wakafa. 50Huu ni mkate ushukao kutoka mbinguni, illi mtu aule wala asife. 51Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele: na mkate nitakaotoa mimi ni nyama yangu nitakayotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. 52Bassi Wayahudi wakashindana wao kwa wao, wakinena; Awezaje mtu huyu kutupa sisi nyama yake tuile? 53Bassi Yesu akawaambia, Amin, amin, nsiwaambieni. Msipoila nyama yake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani jemi. 54Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu ana uzima wa milele; mimi nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maima nyama yangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli, 56Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu, hukaa ndani yangu, na mimi ndani yake. 57Kama vile Baba aishiye alivyonituma mimi, nami naishi kwa ajili ya Baba, kadhalika yeye nae anilae ataishi kwa ajili yangu. 58Huu ni mkale ulioshuka kutoka mbinguni; si kama baba zenu walivyoila manna wakafa; aulae mkate huu ataishi milele. 59Maneno haya aliyasema sunagogini, alipokuwa akifundisha huko Kapenaum.
60Bassi watu wengi katika wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, Neno hili ni gumu, nani awezae kulisikia? 61Yesu akajua nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanaliumigʼunikia neno hili, akawaambia, Neno hili linawachukiza? 62Itakuwaje, bassi, mmwonapo Mwana wa Adamu akijianda huko alikokuwa kwanza? 63Roho ndiyo itiayo uzima; mwili haufai kitu; maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima. 64Lakini kuna wengine miongoni mwemi wasioamini. Maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini na ni nani atakaenisaliti. 65Akanena, Kwa sababu hii nimewaambia ya kwamba hapana mtu awezae kuja kwangu, isipokuwa amejaliwa na Baba yangu. 66Kwa ajili ya haya wengi katika wanafunzi wake wakarejea nyuma, wala hawakuandamana nae tena. 67Bassi Yesu akawaambia wathenashara, Ninyi nanyi mnataka kuondoka? 68Bassi Simon Petro akamjibu, Bwana! twende kwa nani? Wewe una maneno ya uzima wa milele. 69Nasi tumeamini, tena tumejua ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi. 70Yesu akawajibu, Je! sikuwachagua ninyi thenashara, na mmoja wenu ni Shetani? 71Alimnena Yuda, mwana wa Simon Iskariote: maana huyu ndiye atakaemsaliti: nae ni mmoja wa wathenashara.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana MT. 6: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: