Luka MT. 15
15
1BASSI watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia kumsikiliza. 2Mafarisayo na wandishi wakanungʼunika, wakasema, Huyu hukaribisha wenye dhambi, hula pamoja nao. 3Akawaambia mfano huu, akisema, 4Mtu gani wenu aliye na kondoo mia, akipotewa na mmoja, asiyewaacha wale tissa na tissaini jangwani, na kumwendea yule aliyepotea, hatta atakapomwona? 5Bassi amwonapo humweka mabegani mwake, akifurahiwa. 6Nae akija kwake huwaila rafiki zake na jirani zake, huwaambia, Furahini pamoja nami, kwa maana nimemwona kondoo wangu aliyepotea. 7Nawaambieni, Kadhalika itakuwako furaha mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tissa na tissaini, wasiohitaji toba. 8Ama mwanamke gani aliye na rupia kumi, akipotewa na rupia mmoja, asiyewasha taa, na kuifagia nyumba, akitatuta kwa bidii, hatta atakapoiona? 9Bassi, aionapo, huwaita shoga zake na jirani zake, hunena, Furahini pamoja nami, kwa maana nimeiona ile mpia niliyoipoteza. 10Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.
11Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. 12Yule aliye mdogo akamwambia baba yake, Baba, nipe sehemu ya mali iniangukiayo. Akawagawanyia vitu vyake. 13Hatta baada ya siku si nyingi yule mdogo akakusanya vitu vyake vyote, akasafiri kwenda inchi ya mbali: akatapanya huko mali zake kwa maisha ya uasharati. 14Alipokwisha kutumia vyote njaa kuu ikaingia inchi ile, yeye nae akaanza kuhitaji. 15Akaenda akashikamana na mmojawapo wa wenyeji wa inchi ile, nae akampeleka shambani kwake, kulisha nguruwe. 16Akawa akitamani kujishihisha tumbo lake kwa maganda yale waliyokula nguruwe: wala hapana mtu aliyemna kitu. 17Hatta alipojirudia nafsi yake, akasema, Watumishi wa mshahara wangapi wa baba yangu wanakula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. 18Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu, nitamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu, na mbele yako: sistahili kuitwa mwana wako baada ya hayo: 19unifanye kuwa kama mmojawapo wa watumishi wako. 20Akaondoka, akaenda kwa baba yake. Alipokuwa angali mbali, baba yake akamwona, akamhurumia, akapiga mbio, akamwangukia shingoni, akambusu sana. 21Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili baada ya hayo kuitwa mwana wako. 22Lakini baba yake akawaambia watumishi wake, Ileteni joho iliyo bora, mkamvike: mpeni pete kwa kidole chake na viatu kwa miguu yake. 23Kamleteni yule ndama aliyenona, mkamchinje: tukale na kufurahi. 24Kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana. Wakaanza kufanya furaha. 25Bassi, yule mwanawe mkubwa alikuwa shamba, na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, akasikia sauti ya kuimba na kucheza. 26Akamwita mmojawapo wa watumishi wake akamwuliza khabari, Mambo bayo, maana yake nini? 27Akamwambia, Ndugu yako amekuja: na baba yako amemchinja yule ndama aliyenona kwa sababu amempata yu mzima. 28Akakasirika wala hakutaka kuingia: bassi, baba yake akatoka akamsihi. 29Akamjibu baba yake akamwambia, Tazama, mimi nimekutumikia hii miaka mingapi: wala sikukhalifu amri yako wakati wo wote wala hukunipa mimi mwana mbuzi wakati wo wote illi nifurahi pamoja na rafiki zangu. 30Bali alipokuja mwana wako huyo, aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. 31Nae akamwambia, Mwanangu, wewe siku zote u pamoja nami, na vitu vyote nilivyo navyo ni vyako. 32Tena kufanya furaha na kuona furaha kulikuwa wajib, kwa maana huyu ndugu yako alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana.
Iliyochaguliwa sasa
Luka MT. 15: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: