Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka MT. 2

2
1HATTA siku zile kulitoka amri kwa Kaisari Augusto ya kama iandikwe orodha ya majina ya walimwengu wote: 2orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa wakati Kurenio alipotawala Sham. 3Watu wote wakashika njia kwenda kuandikwa, killa mtu mjini kwake. 4Na Yusuf nae akaondoka Galilaya kutoka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Yahudi hatta mji wa Daud, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye wa nyumba na jamaa ya Daud, 5illi aandikwe pamoja na Mariamu mkewe ambae ameposwa nae; nae ana mimba. 6Ikawa katika kukaa kwao huko, siku zake za kuzaa zikatimia. 7Akamzaa mtoto wake wa kifungua mimba, akamfunga nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakuona nafasi katika nyumba ya wageni.
8Katika inchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni usiku na kulinda kundi lao kwa zamu. 9Malaika wa Bwana akawatokea, utukufu wa Bwana ukawangʼaria: wakaingiwa na khohi nyingi. 10Malaika akawaambia, Msifanye khofu; kwa maana nawaletea ninyi khabari njema za furaha kuu, itakayokuwa kwa watu wote: 11maana leo katika mji wa Daud amezaiiwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana. 12Na hii ni ishara kwenu: Mtamkuta mtoto amefungwa nguo za kitoto; amelazwa horini. 13Ghafula hiyo walikuwapo pamoja na yule malaika wengi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, wakisema,
14Utukufu una Mungu palipo juu,
Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.
15Ikawa malaika walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakaambiana, Haya na twende zetu mpaka Bethlehemu, tukaone neno hili lililofanyika, Bwana alilotujulisha. 16Wakaenda kwa haraka, wakamkuta Mariamu na Yusuf, na mtoto amelazwa horini. 17Walipoona wakaeneza khabari za neno waliloambiwa, la huyu mtoto. 18Wote waliosikia wakataajabu kwa yale waliyoambiwa na wachungaji. 19Bali Mariamu aliyahifadhi maneno haya yote akiyatafakari moyoni. 20Wachungaji wakarudi, wakimtukuza Mungu na kumhimidi kwa mambo yote waliyosikia, na waliyoona, kwa namna waliyoambiwa. 21Na zilipotimia siku nane za kumtahiri, alikwitwa jina lake Yesu, lile lililotajwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.
22Nazo siku za kutakasika kwao zilipotimia, kwa sharia ya Musa, wakamleta Yerusalemi, wampe Bwana; 23(kama ilivyoandikwa katika sharia ya Bwana, Killa mume afunguae tumbo la mama yake aitwe mtakatifu kwa Bwana;) 24wakatoe sadaka kama ilivyonenwa katika sharia ya Bwana, Hua wawili, au makinda ya njiwa mawili. 25Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae. 26Nae alikuwa amebashiriwa na Roho Mtakatifu ya kwamba haoni mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27Bassi akaja hekaluni kwa roho: na wazee wake walipomleta mtoto Yesu, wamfanyie kwa desturi ya sharia, 28mwenyewe akampokea mikononi mwake, akimhimidi Mungu, akasema,
29Sasa wamrukhusu, Bwana, mtumishi wako kwa amani,
Kama ulivyosema:
30Kwa kuwa macho yangu yamenona wokofu wako,
31Uuliouweka tayari machoni pa watu wote;
32Nuru ya kuwaangaza mataifa,
Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
33Yusuf na mama yake wakawa wakistaajahu kwa yale yaliyonenwa juu yake; 34Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo; 35hatta na wewe upanga utakupenya roho yako; illi yafumike mawazo ya mioyo mingi. 36Kulikuwa na Auna, nabii mke, binti Fanueli, wa kabila ya Asher; nae kongwe wa siku nyingi, amekuwa na mume miaka saba baada ya ujana wake; 37nae mjane wa miaka themanini na mine; asiyeondoka hekaluni, kwa kufunga na kusali akiabudu usiku na mchana. 38Akitokea yeye nae saa ileile, alimshukuru Mungu, akawapasha khabari zake watu wote waliokuwa wakitazamia ukombozi katika Yerusalemi. 39Nao walipokwisha kuyatimiza yote yaliyomo katika sharia ya Bwana, wakarudi Galilaya hatta mji wao Nazareti, 40Mtoto yule akakua, akaongezeka nguvu, akajazwa hekima; neema ya Mungu ikawa pamoja nae.
41Bassi wazee wake, killa mwaka walikuwa wakienda Yerusalemi siku kuu ya Pasaka. 42Hatta alipopata miaka kumi na miwili, wakapanda kwenda Yerusalemi, kama ilivyokuwa desturi ya siku kuu: 43na wakiisha kuzitimiza siku, walipokuwa wanarudi kwao, yule mtoto Yesu akabaki nyuma Yerusalemi, wala mama yake na Yusuf hawakujua; 44wakadhani yumo katika msafara yao, wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao, 45wasimwone, wakarejea Yerusalemi, wakimtafuta. 46Ikawa baada ya siku tatu, wakamwona hekaluni, ameketi kati ya waalimu, akiwasikiliza, na kuwauliza. 47Wote waliomsikia wakataajahu kwa akili zake na majibu yake. 48Nao walipomwona wakashangaa sana; mama yake akamwambia, Mwanangu, kwani ukatutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. 49Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwa katika nyumba ya baba yangu? 50Wala hawakuelewa na neno lile alilowaanibia. 51Akashuka pamoja nao, akafika Nazareti, akawa anawatii: mama yake akayahifadhi maneno haya yote moyoni mwake. 52Yesu akazidi kuendelea katika hekima, na kimo, na neema kwa Mungu na kwa watu.

Iliyochaguliwa sasa

Luka MT. 2: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia